Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu asema katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran:

Uchapishaji vitabu unapaswa kufuatiliwa kwa bidii kubwa zaidi

Mapema leo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran na kukagua vyumba mbalimbali vya wachapishaji wa vitabu vilivyouzwa kwa wingi. Ayatullah Khamenei ametembelea na kuona kwa karibu vitabu vipya vinavyoonyeshwa katika maonyesho hayo.

Baada ya kutembelea vibanda na vyumba mbalimbali vya maonyesho hayo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alizungumza na wachapishapishaji bora wa vitabu akiwashukuru wadau wa sekta hiyo na kusema kuwa suala la kitabu ni kadhia muhimu isiyokuwa na mbadala. Ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni ubora wa uchapishaji vitabu, idadi yake na maudhui zake zimeongezeka na hali hii haiwezi kulinganishwa na miaka ya huko nyuma. Hata hivyo amesisitiza kuwa bado kuna safari ndefu hadi kufikia hali inayotakikana.

Ameashiria pia suala la kupanuka upeo wa mtazamo wa waandishi na kusema kuwa kumefanyika kazi nzuri katika kuboresha uandishi wa viabu na inatarajiwa kuwa mwenendo huo utaendelea kwa juhudi na uwekezaji mkubwa zaidi.

Ayatullah Khamenei amesema ni muhali kuweza kupatikana maendeleo nchini bila ya kuwepo ustawi katika sekta ya vitabu na kuongeza kuwa Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, taasisi za serikali na watu wenye ari wanapaswa kutoa umuhimu mkubwa kwa maudhui ya kitabu na kufuatilia kwa bidii uandishi wa vitabu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa maendeleo ya Iran katika sekta mbalimbali za uchapishaji na uandishi wa vitabu yanahisika na ametilia mkazo juu ya kupewa umuhimu zaidi sekta hiyo.      

 

 

   

700 /