Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ofisi ya Kiongozi Muadhamu yawataka wananchi wa Iran kutoa misaada kwa wananchi waliokumbwa na baa la njaa Somalia

Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei imewataka wananchi wenye imani na wanaotaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu SW kutoa misaada kwa wananchi waliokumbwa na baa la njaa wa Somalia.

Kufuatia janga la ukame lililolikumba eneo la Pembe ya Afrika hususan Somalia, ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetoa taarifa ikiwataka Wairani wote kuwasaidia Waislamu waliopatwa na baa la njaa wa Somalia katika mwezi huu mtukufu na wenye baraka tele wa Ramadhani.

Matini kamili ya taarifa hiyo ni hii ifuatayo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu.

Katika siku hizi eneo la Pembe ya Afrika hususan nchi iliyokumbwa na masaibu ya Somalia, linashuhudia moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu, na kutokana na ukame, njaa na upuuzaji wa jumuiya za kimataifa, mamilioni ya Waislamu wa Somalia hususan wanawake na watoto wadogo, wanakabiliwa na hatari kubwa.

Kutokana na hali hiyo na kwa kutilia maanani umuhimu mkubwa unaotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa suala la kutolewa misaada kwa watu waliopatwa na masaibu ya njaa huko Somalia, taifa la Kiislamu la Iran linahimizwa kulisaidia haraka taifa la Waislamu wa Somalia katika mwezi huu wenye rehma na baraka na kuwasilisha misaada yake ya kifedha na isiyokuwa ya kifedha kwa wananchi wa Somalia kupitia taasisi husika.

Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu   

700 /