Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa kufa shahidi Mashahidi wa Ghadir:

Kufa shahidi ni taufiki ya Mwenyezi Mungu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema leo katika ujumbe uliotolewa kwa mnasaba wa kuwaenzi mashahidi wa Taasisi ya Jihadi ya Kujitosheleza ya jeshi la Sepah hususan Shahidi Brigedia Jenerali Hassan Muqaddam, kwamba matunda ya watu hawa wema yako katika mikono ya rijali wa jihadi, na watu waliolelewa katika mikono ya rijali hawa wana uwezo wa kudumisha njia yao yenye mwanga na nuru.

Mshahidi hawa 17 walikufa shahidi katika mlipuko uliotokea Jumamosi iliyopita katika kituo cha jeshi la Sepah katika eneo la Malard mkoani Alboz hapa nchini.

Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ni hii ifuatayo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea.

Tukio la kumwagika damu lililotokea katika moja ya vituo vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) ambalo limepelekea kufa shahidi idadi kadhaa ya watu bora wa taasisi hiyo wakiongozwa na kamanda msomi, mchamungu na asiye na majivuno Brigedia Jenerali Hassan Muqaddam, ni tukio chungu na la kuhuzunisha. Mashujaa hawa daima walikuwa wakijitosa katika hatari kwa ujasiri na azma thabiti na kamwe hawakuchoka katika kipindi chote cha vita vya kujitetea kutakatifu na baada yake. Hapana shaka kuwa kufa shahidi yalikuwa matarajio yao makubwa zaidi. Hata hivyo kupoteza rijali adhimu katika nchi na jamii yoyote ile ni hasara na tukio la kusikitisha kwa watu wa nchi hiyo.

Tunashirikiana na familia zao katika msiba huu. Vilevile tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba matunda ya juhudi za rijali hawa yako mikononi mwa wanajihadi, na rijali waliolelewa katika mikono yao wana uwezo wa kudumisha njia hiyo yenye nuru na mwanga.

Wapenzi, fanyeni bidii na hima zaidi kwa kutarajia fadhila zisizokuwa na kikomo za Mwenyezi Mungu na kwa kutawasali kwa roho za mashahidi wenu na muelewe kwamba, kufa shahidi ni taufiki ya Mwenyezi Mungu kwetu sisi na dalili ya baraka na kupandishwa katika daraja za juu.

Ninatoa mkono wa pole kwa familia, marafiki na wale waliokuwa wakifanya kazi na mashahidi hawa.

Sayyid Ali Khamenei

25/Aban/1390  (16/11/11)      

700 /