Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Kuna udharura wa kupanuliwa zaidi anga ya usomaji vitabu hapa nchini

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumapili ametembelea Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran kwa kipindi cha masaa mawili.

Katika shughuli hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, wasimamizi wa vyumba mbalimbali vya maonyesho hayo walitoa maelezo kwa Kiongozi Muadhamu kuhusu vitabu vyao na shughuli za uchapishaji vitabu.

Baadaye Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alihutubia hadhara ya wachapishaji vitabu akiashiria mahudhurio makubwa ya wananchi katika maonyesho hayo ya vitabu na akasisitiza juu ya udharura wa kufanyika mikakati ya kueneza na kupanuliwa zaidi shughuli za usomaji vitabu hapa nchini.

Ayatullah Khamenei amesema kunapaswa kubuniwa mipango madhubuti na kuainishwa malengo ya awamu kadhaa katika kila mwaka sambamba na kufanyika maonyesho ya vitabu na kuzidisha idadi ya watazamaji wa maonyesho hayo pamoja na kupanua zaidi anga ya usomaji vitabu nchini.

Amekumbusha pia udharura wa kuondolewa baadhi ya vizuizi vya uzalishaji na uchapishaji vitabu na kusisitiza kuwa Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu inapaswa kuondoa vizuizi hivyo hususan maudhui ya ughali wa karatasi.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa utengenezaji wa karatasi hapa nchini ni miongoni mwa kazi zenye muda mrefu hapa nchini na amesisitiza kuwa uzalishaji muhimu zaidi wa kitaifa ni ule unaobakia muda mrefu. Amesema njia ya kupanua zaidi usomaji vitabu hapa nchini itafunguliwa kwa kuondolewa baaadhi ya matatizo ya viwanda vya kutengeneza karatasi.

Ayatullah Khamenei amesema maudhuui ya kutarjumiwa vitabu si ya upande mmoja tu na ameongeza kuwa serikali inapaswa kutayarisha uwanja mzuri wa kutarjumiwa vitabu vinavyoandikwa hapa nchini kwa lugha mbalimbali na kufikishwa kwa walimwengu.

Kiongozi wa Mapinduzi yaa Kiislamu amesisitiza juu ya umuhimu wa kusahihishwa vitabu kwa kutilia maanani kanuni za lugha ya Kifarsi na kutilia maanani sura ya kidhahiri ya vitabu na akasema kuwa moja ya kazi muhimu na za dharura katika uzalishaji vitabu ni kuwepo mpangilio mzuri katika ugavi na kuanzishwa maduka ya kuuzwa vitabu hivyo.

Kabla ya hotuba hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, wachapishaji kadhaa walitoa mitazamo yao kuhusu maudhui mbalimbali zinazohusu vitabu na usomaji vitabu.

 

 

 

700 /