Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu katika maeneo yaliyoathiriwa na mtetemeko:

Taifa zima la Iran linaungana na watu waliopatwa na masaibu ya mtetemeko

Kijiji cha Sarand kilichoko katika wilaya ya Haris ndio eneo la kwanza lililotembelewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Baada ya hapo Ayatullah Khamenei alitembelea kijiji cha Kouvich na kuzungumza kwa karibu na wakazi wa kijiji hicho. Amehutubia mkusanyiko wa watu wa eneo hilo akisema kuwa lengo la safari yake katika maeneo yaliyokumbwa na mtetetemeko wa ardhi ni kutoa mkono wa pole na kuonesha mshikamano wake na wananchi wa maeneo hayo. Amesema taifa lote la Iran linashikamana na wakazi wa maeneo yaliyopatwa na masaibu ya mtetemeko wa ardhi.

Ayatullah Khamenei amesema wananchi wa Iran wana umoja na mshikamano na umoja huo ndio sababu ya nguvu, heshima na uwezo wa taifa hili.

Amewausia watu waliopatwa na masaibu ya mtetemeko wa ardhi kuwa na subira na kusema: "Iwapo wakazi wa maeneo haya watashirikiana na kusaidiana, tukio hili linaweza kuwa chombo cha kuleta mabadiliko ya sura ya maeneo haya."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema huduma zilizotolewa hadi sasa kwa watu waliokumbwa na mtetemeko huo zinaridhisha na kuongeza kuwa, maafisa wa serikali wana jukumu zito la kuimarisha na kukarabati nyumba zilizoharibiwa na mtetemeko huo na kwamba wakazi wa maeneo hayo pia wanapaswa kuwasaidia maafisa katika kutekeleza wajibu huo.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kukagua maeneo yaliyokumbwa na mtetemeko wa ardhi kwa kutembelea kijiji cha Bajebaj na kuzungumza kwa karibu na wakazi wake. Vilevile ametembelea vijiji vya Zaghan, Shikhamlo na Urang.

Ayatullah Khamenei ametilia mkazo suala la usimamizi mzuri wa jinsi ya kugawa misaada kwa waathirika wa mtetemeko huo.    

700 /