Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Khamenei katika hotuba za swala ya Idi:

Mabadiliko ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu yanaainisha mustakbali

Siku ya leo ya Idul Fitr, idi ya wampwekeshao Mwenyezi Mungu, Iran imeghiriki katika nuru na uja huku wananchi wa jiji la Tehran wakishiriki kwa wingi katika ibada ya swala ya Idi iliyoongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.

 Katika hotuba za swala ya Idi, Ayatullah Khamenei ameyataja matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni ya kushangaza na yasiyo na kifani. Amesema kuwa, matukio hayo ambayo yanaainisha njia ya mustakbali wa ulimwengu wa Kiislamu yataendelea kwa kasi na mwenendo huo huo kwa baraza zake Mwenyezi Mungu.

Katika hotuba ya kwanza ya swala ya Idul Fitri Ayatullah Khamenei amewapongeza Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya idi na kusema, mwezi wa Ramadhani wa mwaka huu ulikuwa wenye baraka tele kwa rehma zake Allah chini ya kivuli cha dua, ibada na maombi ya wananchi na mahudhurio makubwa ya matabaka mbalimbali ya watu katika mikusanyiko ya kidini hususan katika Usiku za Qadr.

Ameongeza kuwa, kwa baraza za yote hayo kumejitokeza anga ya kimaanawi na kiroho, yenye taathira na itakayobakia hapa nchini ambayo inapaswa kutumiwa vyema. Ayatullah Khamenei amewataka wananchi wote hususan tabaka la vijana kulinda hazina kubwa ya masuala ya kiroho iliyopatikana katika mwezi huo kwa kujiweka karibu zaidi na Qur’ani na kushiriki katika medani za mapambano dhidi ya shetani wa ndani na nje ya nafsi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza harakati nzuri na iliyochuliwa wakati mwafaka ya taifa la Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds (Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani) na akasema kuwa, harakati hiyo adhimu itakuwa na taathira kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ayatullah Khamenei ameashiria hatua ya mataifa ya Kiislamu ya kujiunga na taifa la Iran katika Siku ya Quds na akasema kuwa, mwaka huu mataifa mengi zaidi ya Kiislamu hususan katika nchi zilizopatwa na mwamko wa Kiislamu, yameingia katika medani ya kuitetea Palestina na mwenendo huo utaendelea kwa matakwa yake Mwenyezi Mungu.

Ameyataja maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa ni sawa na kutiririka damu mpya katika mishipa ya umma wa Kiislamu na akasema: “Maandamano ya Siku ya Quds yamepata maana kubwa zaidi kwa kutilia maanani juhudi zinazofanywa siku zote na maadui za kutaka kuwasahaulisha watu kadhia ya Palestina.”

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu yanastaajabisha na hayana kifani. Amongeza kuwa matukio hayo ambayo yanaainisha njia ya mustakbali wa ulimwengu wa Kiislamu yataendelea hivyo hivyo kwa baraza zake Allah.

Amesisitiza kuwa maadui wa umma wa Kiislamu wamejitosa katika medani wakiwa wamejizatiti kwa mbinu tata na nguvu zao zote kwa ajili ya kufelisha mwenendo wa matukio hayo lakini mataifa ya Kiislamu yatabatilisha njama zao.

Ayatullah Khamenei ametilia mkazo udharura wa kutambua kwa kina matukio hayo na kujiepusha na makosa katika uchambuzi wake na akasema kuwa, kila mahala Marekani, Wazayuni na viongozi wa tawala za kidhalimu wanapoanza harakati, basi harakati hiyo huwa ya batili, na umakini katika kuchunguza uhakika huo unatukinga na makosa katika kufanya uchambuzi.

Ameitaja zilzala na mtetemeko wa ardhi uliotokea katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki nchini Iran na kusababisha madhara kwa wananchi kuwa ni tukio chungu na msiba na akaongeza kuwa, taifa zima zimesikitishwa na janga hilo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia kazi za kuridhisha zilizofanyika hadi sasa kwa ajili ya watu waliopatwa na masaibu ya mtetemeko wa ardhi hapa nchini na kusema kuwa, juhudi hizo zinapaswa kudumishwa ili majukumu mazito zaidi kwa ajili ya waliopatwa na maafa hayo yaweze kutekelezwa vyema.

Ayatullah Ali Khamenei amewataka wananchi wazidishe misaada yao kwa walioathiriwa na mtetemeko huo na akasema kuwa, wananchi wa Iran hawawezi kupuuza tukio hilo na wanapaswa kudumisha ushirikiano na maafisa husika katika kuwasaidia watu waliopatwa na maafa.

Amesema kuwa anatarajia athari mbaya za janga hilo zitatoweka kikamilifu kwa hima ya maafisa wa utawala wa Kiislamu na misaada ya wananchi na watu wa maeneo yaliyoathiriwa watashuhudia ukurasa mpya wa ujenzi na ustawi.  

 

 

 

   

 

700 /