Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Jizatitini ili maadui wasithubutu kutoa vitisho dhidi ya Iran
Jizatitini ili maadui wasithubutu kutoa vitisho dhidi ya Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo am...
Vyombo husika viwakamate wahusika wa shambulizi la Ahvaz
Vyombo husika viwakamate wahusika wa shambulizi la Ahvaz
Kufuatia shambulio la kigaidi lililofanywa leo asubuhi katika mji wa Ahvaz kusini magharibi mwa Iran, ambalo limepelekea watu kadhaa kuuawa shahidi na kujeruhiwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mashahidi wa tukio hilo chungu.
Sera za Marekani ni kuanzisha vita na kusababisha mauaji baina ya Waislamu
Sera za Marekani ni kuanzisha vita na kusababisha mauaji baina ya Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe wake uliosomwa leo kwa Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwamba sera za Marekani ni kuchochea vita baina ya Waislamu na akasisitiza kwamba: inapasa kuzizima sera hizo za kishetani kwa umakini na kuwa macho na kwamba Hija na kujibari na washirikina vinawezesha kupatikana umakini huo.
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia hadhara ya Baraza la Idi iliyohudhuriwa na maafisa wa serikali, makamanda wa jeshi, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbalimbali na kusema kuwa, sababu muhimu zaidi za kupelekea kuheshimiwa jamii za Kiislamu duniani ni umoja na kutatua hitilafu zilizopo.
Kuimarishwa vikosi vya jeshi kunalinda taifa
Kuimarishwa vikosi vya jeshi kunalinda taifa
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia uhasama usiokoma wa maadui dhidi ya taifa la Iran na Mfumo wa Kiislamu hapa nchini na kusema kuwa, kukabiliana na mahasimu hao kunahitajia kuimarishwa zaidi uwezo wa jeshi la taifa.
Vijana wenye imani wameipigisha magoti Marekani
Vijana wenye imani wameipigisha magoti Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mapema leo katika hadhara ya maelfu ya wapiganaji wa kujitolea wa jeshi la Basiji waliokwenda kuonana naye kutoka maeneo mbalimbali ya Iran kwamba Basiji ni tukio la aina yake, linalotatua mambo mengi na miongoni mwa mambo ya kijifaharisha ya hayati Imam Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu).
Kuna ulazima wa kudhaminiwa makazi kwa waathirika wa zilzala
Kuna ulazima wa kudhaminiwa makazi kwa waathirika wa zilzala
Baada ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amehutubia kikao cha kushughulikia matatizo ya waathiriwa wa tetemeko hilo kilishoshirikisha maafisa wa kimkoa, viongozi wa kieneo na baadhi ya makamanda wa jeshi na polisi akisema kuwa, viongozi hao wana majukumu mazito ya kushughulikia watu waliopatwa na masaibu ya tetemeko hilo la ardhi mkoani Kermanshah.
Maafisa wa serikali waendelee kuwasaidia waathirika wa zilzala
Maafisa wa serikali waendelee kuwasaidia waathirika wa zilzala
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kusikitishwa sana na tukio chungu la tetemeko la ardhi lililotokea katika mkoa wa Kermanshah huko magharibi mwa Iran na kuwashukuru viongozi wa serikali waliokwenda kwenye maeneo yaliyoathiriwa na tukio hilo na kuonesha mshikamano wao na wananchi.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika kikao na viongozi wa mihimili mitatu ya taifa, yaani vyombo vya Mahakama, Bunge na Serikali kuu.
Taasisi zote ziharakie kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa
Taasisi zote ziharakie kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea magharibi mwa Iran na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kujeruhiwa.
Ayatullah Ali Khamenei ametoa mkono wa pole kwa taifa la Iran hususan watu wa mkoa wa Kermanshah na kuvitaka vyombo vyote vya dola na jeshi kuharakia kuwasaidia watu walioathiriwa na tetemeko hilo.
Baada ya Syria, Iran na Russia zitafanikiwa katika medani nyingine ngumu
Baada ya Syria, Iran na Russia zitafanikiwa katika medani nyingine ngumu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekaribisha pendekezo la Rais Vladmir Putin wa Russia la kupanua zaidi ushirikiano katika nyanja zote na kusema kuwa, kuna udharura wa kutumia tajiriba na uzoefu mkubwa uliopatikana katika miaka ya hivi karibuni kwenye masuala ya kieneo na katika uhusiano wa nchi mbili za Iran na Russia, kuimarisha na kutia nguvu zaidi uhusiano wa pande hizi mbili.

Anwani zilizochaguliwa