Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

IRIB ina jukumu la kustawisha uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu
IRIB ina jukumu la kustawisha uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, ametoa hukumu ambayo ndani yake amemshukuru Mhandisi Izzatullah Zarghami, aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kutokana na jitihada zake kubwa mno na uchapaji kazi wake usiojua kuchoka na amemteua Bw. Mohammad Sarafraz kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Umoja wa Waislamu ni siasa rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu
Umoja wa Waislamu ni siasa rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumanne) ameonana na viongozi na maafisa wa Iran waliosimamia amali ya Hija ya 1435 Hijria na kusema kuwa, ni jambo la dharura mno kuwa na mipangilio mizuri ya kuhakikisha kwamba faida na manufaa ya ibada ya Hija yanakuwa mengi zaidi na zaidi kupitia kuwa na mtazamo wa kimapinduzi na kiubunifu katika kutoa majibu ya mahitaji ya kimaanawi na kifikra ya walengwa na vilevile katika kupambana na shubha na propaganda za uongo zinazoenezwa na maadui dhidi ya Uislamu.
Kutegemea pato la mafuta ni kuweka hatima yetu kwenye mikono ya wapangaji wa bei ya bidhaa hiyo
Kutegemea pato la mafuta ni kuweka hatima yetu kwenye mikono ya wapangaji wa bei ya bidhaa hiyo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumatano) ameonana na mamia ya vijana wenye vipaji wa vyuo vikuu na walioteuliwa kushiriki katika mashindano ya Olympiad na matamasha ya kimataifa na ya ndani na huku akisisitizia udharura wa kuweko silisila kamili iliyoshikamana vyema pamoja na kanali kubwa ya kuzalisha elimu katika Vyuo Vikuu na kwenye vituo vya kielimu na kiutafiti nchini Iran ameongeza kuwa: Iran inapaswa kutumia vizuri vyanzo vyake ilivyo navyo juu ya ardhi yaani akili na vipaji vya vijana wake na watu wenye vipawa nchini kwa ajili ya kuimarisha uchumi wake na sio kutumia vyanzo vyake vyake vilivyo chini ya ardhi na ambavyo vina panda shuka nyingi kama vile mafuta na vyanzo vingine vya chini ya ardhi.
Hali ya sasa ya Iraq ni matokeo ya siasa mbaya za baadhi ya nchi huko Syria
Hali ya sasa ya Iraq ni matokeo ya siasa mbaya za baadhi ya nchi huko Syria
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo alimkaribisha Waziri Mkuu wa Iraq na ujumbe wake ofisi kwake hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo yake na mgeni huyo, Ayatullah Khamenei amesema kuwa usalama, hali bora, uwezo na heshima ya Iraq kama nchi muhimu katika eneo la Mashariki ya Kati, vina umuhimu mkubwa sana kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza uungaji mkono kamili wa Iran kwa serikali mpya ya Iraq na kusema: Hali ya sasa na eneo la Mashariki ya Kati ikiwemo Iraq ni matokeo ya siasa zisizowajibika za madola ya kigeni na baadhi ya nchi za eneo hili huko Syria.
Ushindi wa Ghaza ni bishara ya ushindi mwingine mkubwa zaidi
Ushindi wa Ghaza ni bishara ya ushindi mwingine mkubwa zaidi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na Bw. Ramadhan Abdullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina na ujumbe alioandamana nao na huku akionesha kufurahishwa sana na ushindi wa wananchi wanamapambano wa Ghaza katika vita vya siku 51 vya hivi karibuni na jinsi utawala wa Kizayuni ulivyokiri kushindwa kukabiliana na wananchi hao waliozingirwa kila upande, ameutaja ushindi huo mkubwa kuwa ni dhihirisho la wazi la kutimia ahadi ya nusra ya Mwenyezi Mungu.
Kuzusha hitilafu kati ya Shia na Suni ni kuisaidia Marekani, Uingereza na Uzayuni
Kuzusha hitilafu kati ya Shia na Suni ni kuisaidia Marekani, Uingereza na Uzayuni
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatatu) ameuhutubia mjumuiko mkubwa wa maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali katika Sikukuu ya Ghadir akisema kuwa, kutangazwa Amirul Muuminin Ali kuwa Imam na Uislamu kuzingatia na kuyapa umuhimu masuala ya siasa na utawala ndiyo mambo mawili muhimu ya tukio la Ghadi Khum.
Umoja wa Waislamu, Palestina na tofauti baina ya Uislamu sahihi na wa Kimarekani vipewe kipaumbele
Umoja wa Waislamu, Palestina na tofauti baina ya Uislamu sahihi na wa Kimarekani vipewe kipaumbele
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ametuma ujumbe muhimu kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu Alkaaba akisema kuwa suala la kuwaunganisha Waislamu na kuondoa tofauti baina yao ni jambo lililo na umuhimu mkubwa na kwamba Hija ni dhihirisho la umoja na udugu baina yao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Waislamu wanapokuwa kwenye Hija wanapasa kuzingatia mambo yanayowaunganisha na kuepuka yanayowatenganisha kwa sababu mikono miovu ya wakoloni tokea zamani imekuwa ikifanya njama za kuwatenganisha ili kudhamini maslahi yao haramu katika Umma wa Kiislamu.
Kuisimama kidete kwa taifa la Iran kumewatia ujasiri shakhsia wengi duniani
Kuisimama kidete kwa taifa la Iran kumewatia ujasiri shakhsia wengi duniani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na makamanda wa ngazi za juu wa jeshi na kukitaja kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa zamani wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) kuwa ni nembo ya heshima kwa taifa la Iran.
Iran haitashirikiana na Marekani katika kadhia ya Daesh
Iran haitashirikiana na Marekani katika kadhia ya Daesh
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo ameruhusiwa kuondoka katika Hospitali ya Shahid Rajai mjini Tehran baada ya kukamilisha matibabu na kupata nafuu kikamilifu.
Kabla ya kuondoka hospitali hapo, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alifanyiwa mahojiano na mwandishi habari wa Shirika la Matangazo la Iran (IRIB) akieleza kuridhishwa na upasuaji na matibabu aliyopewa na akasema: “Ninarejea nyumbani nikiwa mzima wa afya ya mwili na mwenye nishati. Ninawashukuru wananchi kwa upendo wao walionionesha katika siku kadhaa zilizopita na ninaona haya na kujihisi mwenye deni zito kwa wananchi.”
Uzalishaji ndiyo ufunguo wa ustawi wa kiuchumi
Uzalishaji ndiyo ufunguo wa ustawi wa kiuchumi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi ameonana na Rais pamoja na wajumbe wa Baraza la Mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kulitaja suala la kuleta utulivu wa kiroho na kisaikolojia katika jamii, kudhibiti mfumuko wa bei na kudhibiti bei ya fedha za kigeni pamoja na kutekeleza mpango wa mfumo wa usalama wa kiafya kuwa ni miongoni mwa kazi zenye thamani na nzuri zilizofanywa na Serikali ya Kumi na Moja ya Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Iran itaamiliana na dunia nzima isipokuwa Marekani na Israel
Iran itaamiliana na dunia nzima isipokuwa Marekani na Israel
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi, (Jumatano) ameonana na Waziri wa Mambo ya Nje, mabalozi na wakuu wa Vitengo vya Utamaduni vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi na kusema kuwa, taasisi ya kidiplomasia ya Iran ni mtetezi aliyeko mstari wa mbele wa malengo na maslahi matukufu ya taifa pamoja na rasilimali za Wairani.
Vilevile amebainisha sifa za kipekee za taasisi ya kidiplomasia ya Iran na udharura wa kuweko udiplomasia amilifu, erevu na unaoangalia mbali katika kipindi hiki muhimu mno cha kuvuka kwenye mfumo mpya wa dunia, na ametoa maelezo muhimu kuhusiana na kutokuwa na faida miamala na mwingiliano na Marekani.
Nchi za Waislamu zinapaswa kutupilia mbali hitilafu zao kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaodhulumiwa wa Ghaza
Nchi za Waislamu zinapaswa kutupilia mbali hitilafu zao kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaodhulumiwa wa Ghaza
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei leo ameonana na mamia ya viongozi na wananchi wa matabaka mbalimbali pamoja na mabalozi wa nchi za Kiislamu walioko nchini Iran na kuwataka Waislamu wote kuwasaidia wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. Amesisitiza kuwa: Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuweka pembeni hitilafu zilizomo ndani yake na Waislamu watumie nguvu zao zote kuwadhaminia mahitaji yao wananchi wa Ghaza.
Dunia nzima inapaswa kuwasaidia kwa silaha wananchi wa Palestina
Dunia nzima inapaswa kuwasaidia kwa silaha wananchi wa Palestina
Mvuto wa sikukuu ya Idul Fitr umeongezeka maradufu leo kutokana na kuswaliwa Swala ya Idi katika kila kona ya Iran ya Kiislamu huku wananchi waumini wenye mshikamano thabiti wa Iran wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye misikiti na maeneo mbalimbali ili kutekeleza ibada hiyo tukufu wakimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa taufiki ya kutimiza mwezi wa taqwa na ibada, mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika ibada hiyo ya kimaanawi ambayo kitaifa imesaliwa katika eneo la "Muswala" wa Tehran, Waislamu wa Tehran wamejumuika kwa wingi kwenye eneo hilo mapema leo asubuhi na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa swala hiyo iliyongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Maafa ya Ghaza yanapaswa kuyaamsha mataifa ya Kiislamu
Maafa ya Ghaza yanapaswa kuyaamsha mataifa ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Jumatatu) ameonana na Rais pamoja na Baraza la Mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuzungumzia kwa muhtasari baadhi ya mafundisho matukufu na aali yaliyomo kwenye kitabu cha Nahjul Balagha na nukta kadhaa za kiakhlaki na kimaadili.
Marekani na Uingereza zimeunga mkono rasmi mauaji ya watoto wa Ghaza
Marekani na Uingereza zimeunga mkono rasmi mauaji ya watoto wa Ghaza
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei leo usiku (Jumamosi) ambayo imesadifiana na usiku wa kukumbuka siku ya kuzaliwa "Karimu Ahlul Bait" Imam Hasan al Mujtaba, AS ameonana na hadhara ya watu wa utamaduni, shaha wa malenga na wahadhiri wa tungo za mashairi na fasihi ya Kifarsi, malenga chipukizi na majimbi wa tungo za kifarsi nchini Iran pamoja na washairi wa lugha hiyo kutoka nchi za Tajikistan, India, Afghanistan na Pakistan.
Lengo la adui ni kuwatumbiza viongozi wa Iran katika makosa ya kimahesabu
Lengo la adui ni kuwatumbiza viongozi wa Iran katika makosa ya kimahesabu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumatatu) ameonana na maafisa, wafanyakazi na majimui ya viongozi wa ngazi za juu wa taasisi mbalimbali za nchi na za kijeshi na sambamba na kubainisha nukta kadhaa muhimu sana zinazohusiana na masuala ya ndani na nje ya Iran amesema kuwa, njama tata na za pande kadhaa za kujaribu kukwamisha na kuharibu mahesabu ya viongozi na taasisisi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndilo lengo kuu la hivi sasa la mabeberu hususan Marekani.
Harakati ya elimu hapa nchini inapaswa kuendelea
Harakati ya elimu hapa nchini inapaswa kuendelea
Mamia ya wahadhiri wa vyuo vikuu vya Iran, alasiri ya leo wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kubadilishana naye mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kielimu, masuala ya vyuo vikuu, ya kiutamaduni, kijamii, kiuchumi na ya kisiasa.
Mwanzoni mwa kikao hicho kilichodumu kwa zaidi ya masaa mawili, wahadhiri saba wa Vyuo vikuu wametoa mitazamo yao tofauti kuhusu masuala mbalimbali.
Baada ya hapo Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia wajibu na umuhimu wa kuiendeleza kwa nguvu zote kasi ya mwamko wa pande zote wa kielimu nchini Iran akiutaja mwamko huo kuwa ndicho kitu kikuu kinachounda mustakbali bora wa Iran na ulimwengu wa Kiislamu

Anwani zilizochaguliwa