Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Qur'ani inaipa jamii ya Kiislamu nguvu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali
Qur'ani inaipa jamii ya Kiislamu nguvu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali
Katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa rehema na mwezi wa kualikwa katika ugeni na Mwenyezi Mungu, mwezi wa msimu wa machipuo wa Qur'ani Tukufu, Husainia ya Imam Khomeini – Mwenyezi mungu amrehemu- leo (Jumapili) ilijaa harufu nzuri ya nuru ya aya za Qur'ani Tukufu. Katika Husainia hiyo pamefanyika mahafali ya Qur'ani Tukufu yaliyowakusanya pamoja maqarii, wahadhiri na mahafidhi wa maneno matukufu ya Allah, ambayo pia yamehudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Hali ya sasa ya Iraq ni vita vya waitifaki wa Marekani dhidi ya wapigania uhuru
Hali ya sasa ya Iraq ni vita vya waitifaki wa Marekani dhidi ya wapigania uhuru
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi ameonana na familia za mashahidi wa Tir 7 (Juni 28) na familia kadhaa za mashahidi na majeruhi wa vita wa mji wa Tehran na kusisitizia haja kubwa ya Iran ya kuelewa na kutekeleza kivitendo risala na ujumbe wa mashahidi. Amesema suala la taifa la Iran kuendeleza njia iliyojaa nuru na matukufu mengi ya mashahidi linaanda uwanja wa kuendelea kuzishinda njama za mabeberu.
Iran inapinga uingiliaji wa Marekani nchini Iraq
Iran inapinga uingiliaji wa Marekani nchini Iraq
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamum Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumapili) ameonana na mkuu na maafisa wa ngazi za juu wa Chombo cha Mahakama na vilevile viongozi wakuu wa mahakama na idara za sheria za makao makuu ya mikoa ya Iran. Amebainisha vipaumbele sita vikuu vya kipindi kipya cha miaka mitano cha uongozi wa Ayatullah Amoli Larijani katika Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, ushirikiano, kupendana na kuwa na sauti moja wakuu wa Mihimili Mitatu Mikuu ya dola (Mahakama, Serikali na Bunge) katika masuala makuu ya nchi na katika kulinda maslahi ya umma ni jambo la dharura sana.
Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu inapaswa kujiepusha na mizozo ya kisiasa
Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu inapaswa kujiepusha na mizozo ya kisiasa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na mkuu, wakurugenzi, wahakiki na watatifi wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu na kusisitiza kuwa, jambo la lazima katika kuendelea kwa njia sahihi na kwa kasi kubwa na harakati ya kielimu ya Iran ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na uongozi na usimamiaji wa kijihadi na vile vile kutia nguvu moyo wa "Sisi tunaweza" sambamba na kulinda misimamo na mielekeo ya kimapinduzi na Kiislamu.
Ayatullah Mishkini alikuwa shakhsia aliyekusanya mambo mengi
Ayatullah Mishkini alikuwa shakhsia aliyekusanya mambo mengi
Leo asubuhi (Alkhamisi), Hujjatul Islam Walmuslimin Mohammad Golpayegani, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesoma matini ya hotuba ya Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na...
Taifa lililo hai la Iran kamwe haliwezi kupigishwa magoti
Taifa lililo hai la Iran kamwe haliwezi kupigishwa magoti
Sambamba na kuwadia mwezi 13 Rajab na maadhimisho matukufu ya siku ya kuzaliwa Bwana wa wanaompwekesha Mwenyezi Mungu, Imam Ali (AS), maelfu ya watu wa matabaka tofauti hasa wananchi wa mkoa wa Ilam wa magharibi mwa Iran leo (Jumanne) wameonana na Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei...
Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran haipaswi kulegeza kamba hata kidogo
Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran haipaswi kulegeza kamba hata kidogo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) ambayo imesadifiana na Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia nchini Iran ameonana na maafisa wa ngazi za juu pamoja na wataalamu bingwa na wasomi wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran na kusema kuwa, moja kati ya mafanikio muhimu zaidi ya maendeleo ya nyuklia ya Iran ni kutia nguvu moyo wa kujiamini kitaifa nchini na kuandaa mazingira ya kupatikana maendeleo ya kielimu katika sekta nyinginezo.

Anwani zilizochaguliwa