Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Fikra potofu za Magharibi kuhusu mwanamke zinapaswa kutupiliwa mbali
Fikra potofu za Magharibi kuhusu mwanamke zinapaswa kutupiliwa mbali
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na mamia ya akina mama bora na wasomi walioteuliwa kutoka kona mbalimbali za Iran na kulitaja suala la kuanzisha kituo kikuu kitakachofanya kazi hadi nje ya mihimili mikuu ya dola kwa ajili ya kupanga mikakati sahihi kuhusiana na kadhia muhimu ya mwanamke na familia, kuwa ni jambo la dharura.
Taifa la Iran limeonesha kuwa linaweza kumshinda adui chini ya kivuli cha umoja, imani na kusimama kidete
Taifa la Iran limeonesha kuwa linaweza kumshinda adui chini ya kivuli cha umoja, imani na kusimama kidete
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumatano alikutana na maelfu ya watu waliokwenda kutembelea maeneo ya operesheni za kuvunja mzingiro wa Abadan huko mashariki mwa Kawavan kusini mwa Iran na kusisitiza juu ya udharura wa kulindwa kumbukumbu, jihadi na kujitolea kwa wapiganaji wa Kiislamu katika maeneo mbalimbali wakati wa vita vya kujitetea kutakatifu.
Iran inapaswa kuwa na nguvu kubwa ya kutetea haki zake mbele ya madhalimu
Iran inapaswa kuwa na nguvu kubwa ya kutetea haki zake mbele ya madhalimu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Ijumaa) ambayo imesadifiana na siku ya kwanza ya msimu wa machipuo na siku ya awali kabisa ya mwaka mpya wa Kiirani wa 1393 Hijria Shamsia ametoa hotuba muhimu mbele ya hadhara na mjumuiko mkubwa na uliojaa hamasa na shauku wa wafanya ziara na majirani wa Haram toharifu ya Imam Ridha AS mjini Mash'had, kaskazini mashariki mwa Iran. Sambamba na kutoa tena mkono wa baraka kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya amebainisha pia vipengee mbalimbali vya ramani kuu ya njia kwa ajili ya Iran katika mwaka huu mpya yaani kaulimbiu ya "Uchumi na Utamaduni wenye Azma ya Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."
Uchumi na utamaduni vinapaswa kupewa umuhimu
Uchumi na utamaduni vinapaswa kupewa umuhimu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameuita mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia ulioanza leo kuwa ni mwaka wa Uchumi na Utamaduni kwa Azma ya Taifa na Utendaji wa Kijihadi.
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia Ayatullah Khamenei amewapongeza Wairani wote dunia kwa mnasaba huo hususan familia za mashahidi na wanaopigana jihadi katika njia ya Uislamu.
Hali ya watu maskini inapaswa kuboreshwa katika maendeleo ya kiuchumi
Hali ya watu maskini inapaswa kuboreshwa katika maendeleo ya kiuchumi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi (Jumanne) amebainisha muundo wa siasa za uchumi wa kimuqawama na imara mbele ya mjumuiko ya mamia ya wakuu na maafisa wa vyombo mbalimbali, wanaharakati wa masuala ya kiuchumi, wakuu wa vituo vya kielimu, vyombo vya habari na taasisi za usimamizi. Amesema kuwa kuna sababu, nia na msukumo na vilevile matarajio ya wananchi kutoka kwa viongozi na maafisa husika.
Viongozi wa Mfumo wa Kiislamu waweke wazi mpaka baina yao na kambi ya adui
Viongozi wa Mfumo wa Kiislamu waweke wazi mpaka baina yao na kambi ya adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na wajumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu) na kutoa hotuba muhimu. Amegusia baadhi ya matukio ya kimataifa na kuzungumza majukumu waliyo nayo viongozi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika wakati huu nyeti na tata.
Jamii yenye utamaduni ya kufa shahidi haiwezi kubakia nyuma
Jamii yenye utamaduni ya kufa shahidi haiwezi kubakia nyuma
Miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na wajumbe wa kamati za Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi, Kongamano la Mashahidi wa Wanachuo na Kongamano la Mashahidi Wasanii, imesambazwa leo asubuhi katika Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mnara wa Milad, jijini Tehran. Mkutano wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wajumbe wa kamati hizo ulifanyika tarehe 16 Februari 2015.
Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mabavu ya Marekani
Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mabavu ya Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia maelfu ya wananchi wa miji mbalimbali ya mkoa wa Azarbaijan Mashariki waliokwenda kuonana naye akilishukuru taifa la Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman (Februari 11) ya kuadhimisha miaka 35 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. Amesema maandamano hayo yalikuwa na ujumbe mbili ambazo ni kusimama kidete na umoja. Ayatullah Khamenei amesema taifa la Iran lilihudhuria kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman katika kujibu ufidhuli, sera za kupenda kujitanua, utovu wa adabu na kiburi cha viongozi wa Marekani, na kutangaza kuwa kamwe halitasalimu amri mbele ya sera za mabavu za Marekani.
Uwezo mkubwa wa nchi hizi mbili unatayarisha uwanja wa kuimarisha uhusiano
Uwezo mkubwa wa nchi hizi mbili unatayarisha uwanja wa kuimarisha uhusiano
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Khamenei amesema udugu, upendo na urafiki uliopo hivi sasa kati ya Iran na Uturuki hauna kifani katika karne za hivi karibuni. Amesema kuwa uwezo mkubwa wa nchi mbili hizi unatayarisha uwanja mzuri wa kupanuliwa na kuimarisha uhusiano.
Umoja ndiyo suala muhimu zaidi la Ulimwengu wa Kiislamu
Umoja ndiyo suala muhimu zaidi la Ulimwengu wa Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapunduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo katika siku ya Maulidi na sherehe za kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) na mjukuu wake Imam Ja'far Swadiq (sa) alikutana na viongozi wa Mfumo wa Kiislamu wa Iran, wageni wanaoshiriki mkutano wa 27 wa Umoja wa Kiislamu na matabaka mbalimbali ya wananchi. Ameuhimiza Umma wa Kiislamu kutimiza matarajio ya Mtume Muhammad (saw) na kusema: Umoja ndiyo suala muhimu zaidi hii leo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Moyo wa jihadi unapaswa kutawala idara zote hapa nchini
Moyo wa jihadi unapaswa kutawala idara zote hapa nchini
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo (Jumatatu) amekaribisha wajumbe wa Baraza la Kiislamu, Meya wa Tehran, manaibu wake, na wakuu wa wilaya tofauti za Tehran. ameashiria ulazima wa kupewa umuhimu maalumu na wa kipekee usanifu majengo wa jiji la Tehran kwa lengo la kuleta mtindo wa Kiislamu wa maisha na kusisitiza kuwa: Kuendesha jiji kubwa kama la Tehran na miji mingine mikubwa nchini kunataka moyo na kujitolea na kuwatumikia wananchi kwa nia ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kwa kutumia elimu na mikakati mizuri.
Mazungumzo ya sasa yamedhihirisha uhasama wa Marekani dhidi ya Iran na Uislamu
Mazungumzo ya sasa yamedhihirisha uhasama wa Marekani dhidi ya Iran na Uislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na maelfu ya maulamaa, wanafikra, wanachuoni na matabaka mbalimbali ya wananchi wa Qum na kusema kuwa moja ya vipengee muhimu vya tukio la tarehe 19 Dei 1356 (Januari 19, 1978) ni kuchukuliwa hatua za kivitendo kwa kutegemea imani thabiti sambamba na kuwa na muono wa mbali tena katika mazingira magumu sana.
Nara ya “Sisi Tunaweza” inapaswa kuimarishwa
Nara ya “Sisi Tunaweza” inapaswa kuimarishwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumanne) ameonana na wajumbe wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni na sambamba na kubainisha umuhimu mkubwa wa suala la utamaduni na nafasi muhimu ya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni ameeleza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na dhamana ya kutekeleza mambo yanayopasishwa na baraza hilo, majukumu ya kusimamia na kuongoza taasisi mbalimbali katika masuala ya utamaduni, udharura wa kuamiliana kwa hekima na masuala ya kiutamaduni, kuzidi kupiga hatua za kielimu katika Vyuo Vikuu, kutunga na kuandaa misingi ya mabadiliko ya kimapinduzi katika sayansi ya jamii na kulindwa mvuto wa lugha ya Kifarsi.
Mafanikio ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia yanapaswa kupongezwa
Mafanikio ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia yanapaswa kupongezwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amejibu barua aliyoandikiwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hujjatul Islam Hassan Rohani kuhusu mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1. Katika barua hiyo Ayatullah Khamenei ameishukuru timu ya Iran katika mazungumzo hayo na kusema kuwa, hapana kwamba taufiki ya Mwenyezi Mungu, dua na uungaji mkono wa taifa la Iran ndizo sababu za mafanikio haya. Ameongeza kuwa, kusimama kidete mbele ya siasa za kutaka kujipanua daima kunapaswa kuwa kielelezo cha njia ya harakati ya maafisa wanaoshughulikia suala hilo.
Iran haitalegeza kamba katika haki zake za nyuklia
Iran haitalegeza kamba katika haki zake za nyuklia
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameiunga mkono timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 mjini Geneva na pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa mistari myekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo hayo.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran wakati alipokutana na makamanda wa Basiji (jeshi la kujitolea la wananchi) kutoka kote Iran. Kikao hicho kimefanyika kwa mnasaba wa Siku ya Basiji.
Hija inapaswa kutumiwa kuzima njama za kuchochea fitina za kimadhehebu
Hija inapaswa kutumiwa kuzima njama za kuchochea fitina za kimadhehebu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatatu) amekutana na kuzungumza na maafisa na wasimamizi wa msafara wa Hija wa Iran akisema kuwa ibada ya Hija ni hadia ya Mwenyezi Mungu na hazina isiyoisha kwa ajili ya kuleta maelewano kuhusu mahitaji ya pamoja ya dunia ya Kiislamu.
Tabasamu ya hadaa ya Marekani isitutumbukize katika makosa
Tabasamu ya hadaa ya Marekani isitutumbukize katika makosa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia mjumuiko mkubwa wa maelfu ya wanafunzi wa shule na vyuo vikuu waliokwenda kuonana naye kwa mnasaba wa Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa akibainisha sababu kuu za uadui wa ubeberu dhidi ya taifa la Iran na kutangaza uungaji mkono wake kwa maafisa wa serikali katika mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1. Amesisitiza kuwa historia ya utendaji wa Marekani inaonesha kuwa, maudhui ya nyuklia ni kisingizio kinachotumiwa kwa ajili ya kudumisha uhasama dhidi ya Iran. Ayatullah Khamenei amesema tabasamu za hadaa za adui hazipaswi kumtumbukiza katika makosa mtu yeyote na kuongeza kuwa, kama mazungumzo hayo ya nyuklia yatakuwa na matunda itakuwa bora la sivyo ushauri wangu ni kuwa, tunapaswa kutazama ndani ya nchi kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali.

Anwani zilizochaguliwa