Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Ayatullah Khamenei awataka wabunge wazingatie uchumi
Ayatullah Khamenei awataka wabunge wazingatie uchumi
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) amekutana na spika pamoja na wabunge wa Majlisi ya 10 ya Ushauri ya Kiislamu ambapo amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa nguvu, hadhi na nafasi ya bunge kuwa kwenye kilele cha mambo yote nchini.
Umapinduzi, njia pekee ya maendeleo na kufikiwa malengo
Umapinduzi, njia pekee ya maendeleo na kufikiwa malengo
Akizungumza leo asubuhi (Ijumaa) mbele ya halaiki kubwa ya matabaka mbalimbali ya wananchi waliofika kuomboleza kwenye Haram ya Imam Khomeini (MA), Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mpainduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa hayati Imam Khomeini (MA) alikuwa mtu muumini, mswalihina na mwanamapinduzi.
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kufunguliwa rasmi duru ya kumi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amewashukuru wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi katika uchaguzi wa bunge hilo na kuwataka wabunge wafanye juhudi za kuhakikisha kuwa uchumi ngangari unafikiwa na pia kuchangia kuimarisha na kueneza utamaduni wa Kiislamu nchini.
Kiongozi Muadhamu aonya dhidi ya upenyaji wa adui
Kiongozi Muadhamu aonya dhidi ya upenyaji wa adui
Ayatullahi Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na mkuu pamoja na wajumbe waliochaguliwa na wananchi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mfumo wa Kiislamu na kusema kuwa baraza hilo kwa hakika ni tukio adhimu. Huku akibainisha utambulisho na njia ya kimapinduzi ya baraza hilo, Kiongozi Muadhamu amesisitiza kwamba njia pekee ya kudumu na kuendelea Mfumo na kuthibiti malengo ya Mapinduzi ni nguvu halisi ya nchi na Jihadi kubwa kwa maana ya kutomfuata adui.
Jukumu la wote katika kukabiliana na upenyaji wa adui ni ubainishaji
Jukumu la wote katika kukabiliana na upenyaji wa adui ni ubainishaji
Sambamba na kuwadia tarehe 3 Khordad sawa na tarehe 23 Mei ambayo ni tarehe ya kukumbukwa operesheni ya kifahari ya Beitul Muqaddas ambayo ilipelekea kukombolewa kwa mji wa Khorramshahr, leo asubuhi (Jumatatu) sherehe za kuhitimu masomo ya makadeti wa Chuo Kikuu cha kijeshi cha Imam Hussein (as) zimefanyika katika uwanja wa chuo kikuu hicho na kuhudhuriwa na Ayatullah Ai Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran.
Kiongozi: Suala la maji ya mito ya mpakani linapasa kutatuliwa
Kiongozi: Suala la maji ya mito ya mpakani linapasa kutatuliwa
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo alasiri (Jumatano) ameonana na kuzungumza na Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan pamoja na ujumbe anaoandamana nao ambapo amaeashiria masuala mengi ya pamoja ya kiitikadi, kiutamaduni na kihistoria yaliyopo kati ya mataifa mawili haya ya Iran na Afghanistan.
Msingi wa ushirikiano imara na wenye manufaa wa Iran na India
Msingi wa ushirikiano imara na wenye manufaa wa Iran na India
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo alasiri (Jumatatu) ameonana na Narendra Damodardas Modi Waziri Mkuu wa India ambapo amaeashiria uhusiano mkongwe, wa muda mrefu na wa kihistoria pamoja na mawasiliano ya kiutamaduni na kiuchumi ya watu wa mataifa haya mawili na kusema kuna nyanja nyingi mno za kuimarishwa uhusiano wa pande mbili hizi.
Marekani ni taghuti na shetani mkubwa
Marekani ni taghuti na shetani mkubwa
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapiduzi ya Kiislamu ya Iran leo Jumatano amewakaribisha washiriki wa duru ya 33 ya mashindano ya kimataifa ya Qurani Tukufu yaliyomalizika ramsi hapa mjini Tehran hapo jana Jumanne.
Ayatullah Khamenei abainisha majukumu matatu makuu ya wanazuoni
Ayatullah Khamenei abainisha majukumu matatu makuu ya wanazuoni
Ayatullah Ali Khameni Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo (Jumamosi) asubuhi amehutubia umati mkubwa wa wakuu, wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vya kidini vya mkoa wa Tehran na kusema kuwa mwongozo wa kifikra na kidini, mwongozo wa kisiasa na uimarishaji mwamko na mwongozo pamoja na madhuhurio katika Nyanja za huduma za kijamii ni majumu matatu muhimu ya wanazuoni.
Usalama ni kipaumbele cha kwanza nchini
Usalama ni kipaumbele cha kwanza nchini
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) amehutubia umati mkubwa wa makamanda na wakuu wa jeshi la polisi nchini na kusema kuwa usalama ni suala la daraja ya kwanza nchini na kusisitiza kwamba wakuu wa jeshi hilo wanapasa kusimamia kikamilifu na kwa nguvu zao zote usalama wa kifikra, kimatendo na kimaadili wafanyakazi wa jeshi hilo pamoja na kudhamini usalama wa kijamii na kimaadili.
Uhusiano wa Iran na Korea Kusini haupaswi kuathiriwa na hila za Marekani
Uhusiano wa Iran na Korea Kusini haupaswi kuathiriwa na hila za Marekani
Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumatatu) ameonana na kufanya mazungumzo na Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Khamenei akiashiria mtazamo chanya wa Jamhuri ya Kiislamu katika suala la kupanua ushirikiano baina yake na nchi za bara la Asia na kulitaja suala la kuwepo mawasiliano ya kudumu baina ya Iran na Korea Kusini kuwa ni jambo lenye manufaa sana kwa nchi zote mbili.
Kutetea Palestina ni nembo ya kutetea Uislamu, utawala wa Kizayuni umepatwa na kiwewe zaidi
Kutetea Palestina ni nembo ya kutetea Uislamu, utawala wa Kizayuni umepatwa na kiwewe zaidi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Jumapili) amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina, Bwana Ramadhan Abdullah Shallah na ujumbe unaoandamana naye. Ayatullah Khamenei ametoa uchanganuzi kamili kuhusu hali ya sasa ya Mashariki ya Kati na kusema kuwa, hali hii ni jitihada za kambi ya Magharibi inayoongozwa na Marekani kwa ajili ya kulidhibiti eneo hili kupitia njia ya vita kubwa na pana dhidi ya kambi ya Uislamu. Amesisitiza kuwa, vita kubwa inayoendelea sasa katika eneo hili ni mwendelezo wa vita vilivyoanza miaka 37 iliyopita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na katika mpambano huo suala la Palestina ni suala la asili na kuu.
Ayatullah Khamenei: Marekani inawaogopesha wawekezaji wa kigeni kuwekeza Iran
Ayatullah Khamenei: Marekani inawaogopesha wawekezaji wa kigeni kuwekeza Iran
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi (Jumatano) katika kuwadia Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambayo ni Mei Mosi amekutana na maelfu ya wafanyakazi na huku akiisifu jamii ya wafanyakazi nchini kutokana na uaminifu na uthabiti wao kwa Mapinduzi na Mfumo wa Kiislamu, amesisitiza juu ya kutatuliwa matatizo yao, kuimarishwa uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi, udharura wa kupambana vilivyo na magendo ya bidhaa na kuzuiwa uagizaji kutoka nje wa bidhaa ambazo ni sawa na zile zinazozalishwa ndani ya nchi.
Kuna udharura wa kukabiliana na vizuizi vya madola ya kibeberu dhidi ya nchi zinazojitawala
Kuna udharura wa kukabiliana na vizuizi vya madola ya kibeberu dhidi ya nchi zinazojitawala
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumapili) amemkaribisha na kuzungumza na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambako amesisitizia udharura wa kuzidishwa ushirikiano wa aina zote katika nyuga za kiuchumi na kisiasa. Amesema kuwa, ushirikiano wa nchi huru na zinazojitawala unapaswa kuimarishwa kadiri inavyowezekana na nchi hizo inabidi zizidi kukurubiana licha ya baadhi ya madola ya kibeberu kufanya njama za kukwamisha jambo hilo.
Kupambana na vita laini kunahitajia malezi ya vijana wa kimapinduzi na wenye azma thabiti
Kupambana na vita laini kunahitajia malezi ya vijana wa kimapinduzi na wenye azma thabiti
Akizungumza leo asubuhi (Jumatano) na maelfu ya wanachama wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi kutoka kote nchini, Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiiskamu amesema kuwa moja ya medani muhimu za Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kukabiliana na kambi ya uistikbari ni suala la vijana na kusisitiza kuwa, kambi iliyo mkabala na Mfumo wa Kiislamu inataka kubadilisha utambulisho wa kidini na kimapinduzi wa vijana wa Kiirani na kuondoa miongoni mwao matumaini, uchangamfu na motisha.
Matunda ya mazungumzo hayahisiki katika safari za viongozi wa Ulaya nchini Iran
Matunda ya mazungumzo hayahisiki katika safari za viongozi wa Ulaya nchini Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumanne) ameonana na kufanya mazungumzo na Bw. Matteo Renzi, Waziri Mkuu wa Italia hapa mjini Tehran. Amegusia historia ya uhusiano mzuri baina ya nchi mbili za Iran na Italia tangu huko nyuma na namna nchi hizo mbili zinavyokaribisha kuongezwa wigo wa ushirikiano huo na kusema kuwa, tatizo na udhaifu wa safari za mara kwa mara za hivi karibuni za viongozi wa Ulaya nchini Iran ni kule kushindwa kuonekana matunda ya kivitendo na ya waziwazi ya mazungumzo na safari hizo.
Marekani na madola yanayodai kupambana na ugaidi hayasemi ukweli katika uwanja huo
Marekani na madola yanayodai kupambana na ugaidi hayasemi ukweli katika uwanja huo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumatatu) ameonana na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan ambapo amegusia udharura wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi mbili katika nyuga tofauti za kisiasa, kiuchumi, kimataifa na katika vita dhidi ya ugaidi. Amesema kuwa: Baadhi ya madola hususan Marekani si wakweli katika madai yao ya kupambana na ugaidi, lakini nchi za Kiislamu zinaweza kupambana vilivyo na vitisho vyote vinavyoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa kuwa na ushirikiano wa kweli baina yao.

Anwani zilizochaguliwa