Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Maafa ya kusikitisha ya Mina hayapasi kusahauliwa
Maafa ya kusikitisha ya Mina hayapasi kusahauliwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo (Jumatatu) ameonana na maafisa wa kusimamia ibada ya Hija wa Iran na kuyataja maafa machungu mno na ya kusikitisha sana ya Mina kuwa ni miongoni mwa mitihani ya Mwenyezi Mungu. Amezilaumu tawala za nchi mbalimbali na hususan tawala za nchi za Magharibi na mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu kwa kunyamazia kimya msiba huo mkubwa kusisitiza kuwa: Tukio hilo halipaswi kabisa kusahauliwa na kwamba chombo cha diplomasia na Taasisi ya Hija ya Iran vina wajibu wa kulifuatilia ipasavyo suala hilo.
Kubakia hai malengo na nara za Mapinduzi kunamkasirisha adui
Kubakia hai malengo na nara za Mapinduzi kunamkasirisha adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumatano) amehutubia hadhara ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana wenye vipaji bora vya kielimu nchini akitoa nasaha na tahadhari muhimu kwa watu wenye vipawa na viongozi nchini. Pia amesisitizia ulazima wa kuipa uzito wa hali ya juu taasisi ya watu wenye vipawa ikiwa ni taasisi ya kitaifa na ya kiistratijia na vilevile kuandaa uwanja wa kuchanua na kutoa msaada wa kielimu vijana hao wenye vipaji katika jamii. Amesema, mashirika ya elimu za kimsingi ni miongoni mwa nguzo kuu za uchumi ngangari na wa kusimama kidete.
Lengo kuu la vita laini vya adui ni kubadili hakika ya Jamhuri ya Kiislamu na itikadi za wananchi
Lengo kuu la vita laini vya adui ni kubadili hakika ya Jamhuri ya Kiislamu na itikadi za wananchi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatatu) amehutubia hadhara ya viongozi na wakurugenzi wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na wajumbe wa baraza linalosimamia utendji wa shirika hilo akieleza malengo ya vita laini iliyoratibiwa, kubwa na ya pande zote ya mfumo wa ubeberu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Amesema kubadilisha itikadi za wananchi ndiyo lengo muhimu zaidi la vita hivyo tata. Ametilia mkazo nafasi ya kipekee ya IRIB katika mpambano huo mkubwa, na kusisitiza udharura wa kuwepo mipango mizuri na ya kitaalamu kwa ajili ya kutimiza majukumu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.
Ni marufuku kuzungumza na Marekani kwa sababu ya madhara yake mengi
Ni marufuku kuzungumza na Marekani kwa sababu ya madhara yake mengi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatano) amehutubia hadhara ya makamanda na wafanyakazi wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), familia zao na familia za mashahidi wa jeshi hilo. Ameashiria nafasi na mchango wa vijana wanamapinduzi wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Sepah na vijana shupavu wa kusini katika kulinda usalama wa baharini na kumtia woga adui na akasema: Maadui wanataka kubadilisha mahesabu ya maafisa wa Iran na kubadili fikra za wananchi hususan vijana hivyo wananchi wote wanapaswa kuwa macho na makini.
Imarisheji jeshi kiasi kwamba adui asifikirie kuishambulia Iran
Imarisheji jeshi kiasi kwamba adui asifikirie kuishambulia Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Akhamisi) amehutubia hadhara ya makamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kusema, sababu ya uadui unaofanywa dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kusimama kidete kwa taifa la Iran, uwazi na kutosalimu amri kwake mbele ya siasa za ubeberu. Amesisitiza kuwa vikosi vya jeshi la Iran vinapaswa kuzidisha kasi ya maendeleo na kuzidisha utayarifu wake kwa kadiri kwamba, adui asithubutu hata kuwa na fikra ya kuihujumu Iran.
Kuna ulazima wa kuundwa kamati ya kuchunguza tukio la Mina
Kuna ulazima wa kuundwa kamati ya kuchunguza tukio la Mina
Ayatullah Khamenei ameashiria tukio la kusikitisha la Mina huko Saudi Arabia na kusema tukio hilo ni msiba halisi kwa taifa la Iran kutokana na kufariki dunia maelfu ya mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu hususan mamia ya mahujaji wa Kiirani. Ameashiria udharura wa kuundwa kamati ya kutafuta ukweli kuhusu tukio hilo itakayoshirikisha nchi za Kiislamu ikiwemo Iran na kusema: Serikali ya Saudi Arabia haitekelezi majukumu yake katika suala la kusafirisha miili mitoharifu ya mahujaji wa Iran waliofariki dunia na hadi sasa Jamhuri ya Kiislamu imelinda heshima ya udugu katika ulimwengu wa Kiislamu kwa kuonesha uvumilivu na adabu ya Kiislamu; lakini pia wanapaswa kutambuwa kwamba, utovu wa heshima wa aina yoyote ile kwa makumi ya maelfu ya mahujaji wa Iran walioko Makka na Madina na kutotekeleza majukumu yao kwa ajili ya kusafirisha miili mitoharifu ya mahujaji wa Iran kutakabiliwa na jibu kali na la kuumiza.
Waislamu hawatasahau maafa ya Mina
Waislamu hawatasahau maafa ya Mina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mapema leo mwanzoni mwa darsa yake fiqhi kuwa Ulimwengu wa Kiislamu una maswali mengi ya kuuliza kuhusu maafa yaliyotokea Mina nchini Saudi Arabia na kwamba watawala wa nchi hiyo wanapaswa kuuomba radhi Umma wa Kiislamu na familia zilizopatwa na msiba badala ya kuzituhumu pande nyingine; vilevile watalawa wa Saudia wanapaswa kukubali jukumu na kuhusika kwao na maafa hayo makubwa na kushughulikia taathira zake.
Serikali ya Saudi Arabia inapaswa kubeba dhima kubwa ya tukio hilo chungu
Serikali ya Saudi Arabia inapaswa kubeba dhima kubwa ya tukio hilo chungu
Kufuatia maafa yaliyosababisha msiba mkubwa hii leo huko Mina, Saudi Arabia, ambapo idadi kubwa ya Wageni wa Mwenyezi Mungu wameaga dunia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe akieleza mshikamano wake na watu waliopatwa na msiba katika tukio hilo la kusikitisha na kutoa mkono wa taazia kwa familia zao. Vilevile Ayatullah Ali Khamenei ametangaza siku tatu za maombolezo ya taifa nchini Iran.
Siasa zilizojaa shari za Marekani na jinai za utawala wa Kizayuni vinapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza cha Waislamu
Siasa zilizojaa shari za Marekani na jinai za utawala wa Kizayuni vinapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza cha Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu akisema kuwa siasa zilizojaa shari za ubeberu za kuanzisha matatizo makubwa kwa Umma wa Kiislamu na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni na kuvunjiwa heshima Msikiti wa al Aqsa ndio suala lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa Waislamu wote. Ametoa wito kwa maulama na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kutekeleza majukumu yao mbele ya matukio hayo na kusema: Na Hija na mikusanyiko yake mikubwa ya Waislamu, ni mahala bora zaidi pa kujitokeza na kukabidhiana jukumu hilo la kihistoria, na fursa ya kujibari na kujitenga na washirikina ni mojawapo ya minasaba adhimu ya kisiasa inayopaswa kutumiwa vyema.
Ayatullah Khamenei ameashiria tukio la kusikitisha la kufariki dunia idadi kadhaa ya mahujaji ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka na majukumu makubwa ya kudhamini usalama wa Wageni wa Mwenyezi Mungu Rahmani na kusisitiza kuwa: Takwa letu kubwa ni kutekelezwa jukumu hilo.
Walemavu wa vita ni picha ya kipindi cha mtihani mkubwa wa taifa la Iran wakati wa vita vya kijihami
Walemavu wa vita ni picha ya kipindi cha mtihani mkubwa wa taifa la Iran wakati wa vita vya kijihami
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumapili) kabla ya kuanza Wiki ya Kijihami Kutakatifu hapa nchini amekutana na kufanya mazungumzo kwa karibu na walemavu wa vita na familia zao na kuwajulia hali. Amesema kuwa: Vilema wa vita ni picha ya kipindi cha mtihani mkubwa wa taifa la Iran wakati wa vita vya kujihami kutakatifu na kuwepo vilema hao katika jamii kwa hakika kunabainisha uhakika wa kihistoria, kimaarifa, kisiasa na kimataifa.
Adui anataka kubadili itikadi za jamii na kuwa na ushawishi nchini Iran
Adui anataka kubadili itikadi za jamii na kuwa na ushawishi nchini Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na maelfu ya makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kulitaja jeshi hilo kuwa ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu na ni la walinzi waliomacho na wenye welewa mkubwa na ni jicho la Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya ndani na nje ya Iran.
Utawala wa Kizayuni wa Israel hautakuwepo tena baada ya miaka 25
Utawala wa Kizayuni wa Israel hautakuwepo tena baada ya miaka 25
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) amehutubia mjumuiko mkubwa wa maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali ambapo ameonya kuhusu njama za Marekani za kutaka kujipenyeza katika baadhi ya masuala ndani ya Iran. Ameutaja uchumi wenye nguvu na ngangari, maendeleo na ustawi endelevu wa kielimu na kulindwa na kuimarishwa moyo wa kimapinduzi hususan baina ya vijana kuwa ni mambo matatu muhimu ya kuweza kukabiliana kwa umakini na kwa nguvu zote na uadui usio na mwisho wa Shetani Mkubwa, Marekani.
Si mantiki kwa baadhi ya nchi za Ulaya kufuata kibubusa sera za Marekani
Si mantiki kwa baadhi ya nchi za Ulaya kufuata kibubusa sera za Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya leo alimkaribisha ofisini kwake Rais Heinz Fischer wa Austria aliyeko safarini hapa nchini. Katika mazungumzo yake na mgeni huyo, Ayatullah Ali Khamenei ameashiria uadui wa serikali ya Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na Washington kupoteza maslahi yake hapa nchini Iran na kusisitiza kuwa, si jambo la mantiki kwa baadhi ya nchi za Ulaya kufuata kibubusa sera za kihasama za Marekani dhidi ya Iran. Hata hivyo amesema Austria si miongoni mwa nchi hizo.
Kuna udharura wa kuzalisha bidhaa za Kiislamu zenye mvuto
Kuna udharura wa kuzalisha bidhaa za Kiislamu zenye mvuto
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo (Jumatatu) ameonana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na wajumbe wa Baraza Kuu la Masuala ya Intaneti la Iran na kulitaja baraza hilo kuwa ndicho kituo kikuu cha kuweka sera kwa uangalifu mkubwa, kwa kuzingatia majukumu na kwa kujiamini kuhusiana na masuala ya intaneti. Ameashiri kuzidi kukua na kupanuka kwa kasi kubwa suala hili la kipekee la Intaneti amesisitiza kuwa: kuna ulazima wa kutumia uwezo na vipaji vya vijana nchini Iran na kwa kubuni sera sahihi na hatua makini na zenye uratibu mzuri wa pamoja tena bila ya kupoteza muda, kupigwe hatua za haraka na za maana za kutoka katika hali ya kusubiri kutoa radiamali katika uga wa Intaneti na kuingia kwa nguvu zote kwenye medani hiyo kwa lengo la kuwa na taathira kubwa, nzuri na kuzalisha masiala ya Kiislamu yenye umakini na mvuto mkubwa.
Kuimarisha uhusiano wa nchi za Kiislamu ndiyo njia pekee ya kuondoa shari ya madola ya kibeberu
Kuimarisha uhusiano wa nchi za Kiislamu ndiyo njia pekee ya kuondoa shari ya madola ya kibeberu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Jumamosi) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Almazbek Atambayev wa Kyrgyzstan aliyeko safarini hapa nchini.
Katika mazungumzo hayo Kiongozi Muadhamu amesisitiza udharura wa kuimarishwa zaidi uhusiano wa pande mbili kati ya nchi ndugu na za Waislamu na kusisitiza kuwa: Msingi wa siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ni kuzidisha uhusiano na mfungamano wa pande zote na imara baina ya nchi ndugu za Kiislamu.
Viongozi wa serikali wanapaswa kujibu rasmi matamshi mabaya ya maafisa wa Marekani
Viongozi wa serikali wanapaswa kujibu rasmi matamshi mabaya ya maafisa wa Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Alkhamisi) amekutana na wawakilishi wa Baraza la Wataalamu na kulitaja baraza hilo kuwa ni dhihirisho kamili la demokrasia ya Kiislamu na sababu ya sakina na utulivu katika jamii. Amewausia maafisa wote hapa nchini kufanya harakati na juhudi katika fremu ya mfumo wa fikra wa Kiislamu na kuchunga wasije kutumbukia katika sera za mfumo wa kibeberu au kuwa bamba lake la kupigia muhuri. Amesema kuwa wadhifa muhimu zaidi wa maulama wa dini, wasomi wa vyuo vikuu na maafisa wa utawala ni kuwa macho zaidi kuhusu mipango ya adui, kuitambua na kueleza mustakbali unaotia matumaini na wenye maendeleo ya nchi katika fremu ya vigezo vya mfumo wa kifikra wa Uislamu, kwa kutumia uwezo na vipawa vya vijana na uwezo wa taifa.
Uadui wa Marekani haujapungua, inafanya jitihada za kupenya Iran
Uadui wa Marekani haujapungua, inafanya jitihada za kupenya Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatano) amekutana na baraza la mawaziri likiongozwa na Rais Hassan Rouhani ambako amesema kuwa falsafa ya siku hizi za kukumbuka tukio la kuuawa shahidi Mohammad Ali Rajaei na Mohammad Javad Bahonar (Rais na Waziri Mkuu wa zamani wa Iran) kupewa jina la Wiki ya Umoja ni kubakisha hai vigezo vya kifikra, kimwenendo na kishakhsia vya mashahidi hao mawili azizi.
Uzoefu wa umoja wa taifa la Iran upelekwe Hija
Uzoefu wa umoja wa taifa la Iran upelekwe Hija
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi (Jumamosi) amezungumza mbele ya hadhara ya wasimamizi na wafanyakazi wa Taasisi ya Hija na Ziara za Maeneo Matakatifu na kusema kuwa hija inadhamini 'kudumu kwa Uslamu' na ni nembo ya 'umoja na utukufu' wa Umma wa Kiislamu. Amesisitiza juu ya uzingatiaji sambamba upande wa kijamii na wa mtu binafsi wa ibada hiyo kubwa na kusema kuwa kuhamishiwa katika mkusanyiko adhimu wa hija, uzoefu wa umoja wa taifa la Iran kutauletea Umma wa Kiislamu mshikamano, umoja na nguvu zaidi.
Jamhuri ya Kiislamu inazinyooshea mkono wa urafiki serikali za Kiislamu
Jamhuri ya Kiislamu inazinyooshea mkono wa urafiki serikali za Kiislamu
Akizungumza Leo asubuhi (Jumatatu) mbele ya hadhara ya wanazuoni, wananadharia, na wageni wa kikao cha Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as) na vilevile wageni wa kikao cha Muungano wa Redio na Televisheni za Kiislamu, Ayatullahil Udhma Khamenei Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mapambano dhidi ya njama za uistikbari katika eneo (Mashariki ya Kati) ni misdaki ya wazi (kusudio halisi) ya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Anwani zilizochaguliwa