Habari

Jizatitini ili maadui wasithubutu kutoa vitisho dhidi ya Iran Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo am...

Fikisheni ujumbe wa kisiasa wa Hija kwa Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu adhuhuri ya leo amekutana na kuzungumza na maafisa wanaosimamia ibada ya Hija wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia hadhara ya Baraza la Idi iliyohudhuriwa na maafisa wa serikali, makamanda wa jeshi, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbalimbali na kusema kuwa, sababu muhimu zaidi za kupelekea kuheshimiwa jamii za Kiislamu duniani ni umoja na kutatua hitilafu zilizopo.

Moyo ya kishujaa, kujitolea na imani ni kinga mbele ya uadui wa maadui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu adhuhuri ya leo amekutana na baadhi ya familia za mashahidi watukufu na kusema kuwa heshima, usalama na maendeleo ya Iran yametokana na kujitolea na kujitoa mhanga kwa mashahidi.

Kuimarishwa vikosi vya jeshi kunalinda taifa
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia uhasama usiokoma wa maadui dhidi ya taifa la Iran na Mfumo wa Kiislamu hapa nchini na kusema kuwa, kukabiliana na mahasimu hao kunahitajia kuimarishwa zaidi uwezo wa jeshi la taifa.

Sharti la mafanikio ni kuunganisha sayansi za jamii na misingi ya kidini
Hotuba iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 22 Mei (Khordad Mosi, 1396 Hijria Shamsia) kwa wasimamizi na watayarishaji wa Kongamano la Kimataifa la Qur'ani na Sayansi za Jamii (Humanities) imesomwa mapema leo katika kongamano hilo katika mji mtakatifu wa Qum.

Vijana wenye imani wameipigisha magoti Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mapema leo katika hadhara ya maelfu ya wapiganaji wa kujitolea wa jeshi la Basiji waliokwenda kuonana naye kutoka maeneo mbalimbali ya Iran kwamba Basiji ni tukio la aina yake, linalotatua mambo mengi na miongoni mwa mambo ya kijifaharisha ya hayati Imam Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu).

Kuna ulazima wa kudhaminiwa makazi kwa waathirika wa zilzala
Baada ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amehutubia kikao cha kushughulikia matatizo ya waathiriwa wa tetemeko hilo kilishoshirikisha maafisa wa kimkoa, viongozi wa kieneo na baadhi ya makamanda wa jeshi na polisi akisema kuwa, viongozi hao wana majukumu mazito ya kushughulikia watu waliopatwa na masaibu ya tetemeko hilo la ardhi mkoani Kermanshah.

Maafisa wa serikali waendelee kuwasaidia waathirika wa zilzala
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kusikitishwa sana na tukio chungu la tetemeko la ardhi lililotokea katika mkoa wa Kermanshah huko magharibi mwa Iran na kuwashukuru viongozi wa serikali waliokwenda kwenye maeneo yaliyoathiriwa na tukio hilo na kuonesha mshikamano wao na wananchi.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo katika kikao na viongozi wa mihimili mitatu ya taifa, yaani vyombo vya Mahakama, Bunge na Serikali kuu.

Baada ya Syria, Iran na Russia zitafanikiwa katika medani nyingine ngumu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekaribisha pendekezo la Rais Vladmir Putin wa Russia la kupanua zaidi ushirikiano katika nyanja zote na kusema kuwa, kuna udharura wa kutumia tajiriba na uzoefu mkubwa uliopatikana katika miaka ya hivi karibuni kwenye masuala ya kieneo na katika uhusiano wa nchi mbili za Iran na Russia, kuimarisha na kutia nguvu zaidi uhusiano wa pande hizi mbili.

Tukabiliane na wapinzani wa uhusiano wa Iran na Azerbaijan
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa kuna wanaopinga uhusiano wa karibu na wa udugu baina ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan, na kwa msingi huo kuna ulazima wa kukabiliana na wanaotekeleza njama hizo.

Siri ya ushindi wa hivi karibu Iraq ni umoja na jihadi ya vijana waumini
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa umoja wa kaumu mbalimbali na himaya ya serikali ya Iraq kwa makundi ya wananchi na vijana waumini na mashujaa ndiyo siri ya ushindi uliopatikana hivi karibuni nchini humo dhidi ya makundi ya kigaidi na wasaidizi wao.

Utawala wa Kizayuni unataka kuunda Israel mpya katika eneo hili
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo usiku ameonana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na ujumbe alioandamana nao hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba kuna ulazima wa kuzidishwa kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi wa nchi mbili.

Maadui wanafanya njama za kuzuia jihadi ya taifa la Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na familia ya Shahidi Muhsin Hojaji na kumtaja shahidi huyo kuwa ni msemaji wa mashahidi waliodhulumiwa na kukatwa vichwa. Ameashiria mahudhurio makubwa ya wananchi katika mazishi ya shahidi huyo na kusema: Mwenyezi Mungu SW amelipa izza na fahari taifa la Iran kupitia jihadi ya Muhsin azizi na amemfanya kuwa nembo ya kizazi cha vijana wa kimapinduzi na muujiza wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Hija ni fursa bora zaidi kwa ajili ya kuzima propaganda za maadui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuna kambi kubwa ya kimataifa ya propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kwamba: Fursa ya Hija ni minbari bora kabisa ya tablighi kwa ajili ya kujenga mawasiliano na walimwengu na kuzima propaganda za upande wa pili.
