Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Kongamano Kubwa la Hijja Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu ...
Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba tukufu ya Allah
Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba tukufu ya Allah
Katika kuwadia msimu wa ibada tukufu ya Hija, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbu muhimu kwa mnasaba huu kwa Waislamu wote duniani na hasa kwa Mahujaji wanaozuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al-Kaaba huko katika mji mtakatifu wa Makka. Amesema Hija ya Nabii Ibrahim (as) ni dhihirisho la izza na utukufu wa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na madhalimu wa kimataifa. Huku akiashiria matukio machungu ya maafa ya Mina mwaka uliopita, amezihutubu serikali na mataifa ya Kiislamu kwa kusisitiza kuwa ulimwengu wa Kiislamu zikiwemo serikali na mataifa ya Waislamu unapasa kuwafahamu vyema watawala wa Saudia na kuwawajibisha kutokana na jinai ambazo wamezieneza katika ulimwengu wa Kiislamu, na wakati huohuo kufikiria juu ya njia za msingi za kusimamia Haram Mbili Takatifu na suala zima la Hija. Ufuatao ni ujumbe kamili wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kufunguliwa rasmi duru ya kumi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amewashukuru wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi katika uchaguzi wa bunge hilo na kuwataka wabunge wafanye juhudi za kuhakikisha kuwa uchumi ngangari unafikiwa na pia kuchangia kuimarisha na kueneza utamaduni wa Kiislamu nchini.
Mwaka mpya ni mwaka wa Uchumi Ngangari, Hatua na Vitendo
Mwaka mpya ni mwaka wa Uchumi Ngangari, Hatua na Vitendo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa kuanza mwaka mpya wa 1395 Hijria Shamsia akiwapa mkono wa kheri ya mwaka mpya na Nairuzi wananchi wote na Wairani hususan familia tukufu za mashahidi na majeruhi wa vita. Vilevile amewakumbuka na kuwaenzi mashahidi na Imam Khomeini na kusema: “Mwaka mpya ninaupa jina la Mwaka wa Uchumi Ngangari, Hatua na Vitendo”.
Ujumbe wa tanzia baada ya kufariki dunia Salahshoor
Ujumbe wa tanzia baada ya kufariki dunia Salahshoor
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe wa tanzia kufuatia kufariki dunia mtengeneza filamu mkubwa na mashuhuri na msanii aliyeshikamana vizuri na dini, marehemu Bw. Farajollah Salahshoor. Matini ya jumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni hii ifuatayo:
Matunda haya yamepatikana kutokana na kusimama imara
Matunda haya yamepatikana kutokana na kusimama imara
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amejibu barua ya Rais Hassan Rouhani kuhusiana na kumalizika mazungumzo ya nyuklia ambapo ameelezea kufurahishwa kwake na matunda ya kusimama imara taifa la Iran mbele ya vikwazo vya kidhalimu na kurudi nyuma pande zilizokuwa zinakabiliana na Iran kutokana na jitihada za wasomi na wanasayansi wa nyuklia wa Iran na jitihada za watu wote waliohusika kwenye mazungumzo hayo. Ayatullah Khamenei amesisitiza na kutilia mkazo nukta tano muhimu katika barua hiyo iliyotumwa kwa Rais Hassan Rouhani.
Matini kamili ya majibu hayo ni hii ifuatayo:
Azma kubwa ya vijana na wanachuo ndiyo njia pekee ya kubatilisha njama za adui
Azma kubwa ya vijana na wanachuo ndiyo njia pekee ya kubatilisha njama za adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, ametoa ujumbe kwa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya barani Ulaya na kusema kwamba, kuwa na nia na azma ya kweli na kufanya jitihada zilizosita vijana wote na wanachuo wa Iran ndiyo njia pekee ya kufelisha njama za kambi ya adui iliyosimama kukabiliana na Iran ya Kiislamu.
Jengeni misingi ya kuamiliana kwa njia sahihi na ulimwengu wa Kiislamu
Jengeni misingi ya kuamiliana kwa njia sahihi na ulimwengu wa Kiislamu
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewaandikia barua vijana wa nchi za Magharibi akisema kuwa, matukio machungu ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa yameandaa uwanja wa kutafakari kwa pamoja kuhusu njia ya utatuzi wa migogo ya sasa. Amebainisha mifano ya kuhuzunisha ya athari mbaya za ugaidi unaoungwa mkono na baadhi ya madola makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu, uungaji mkono wao kwa ugaidi wa kiserikali wa sefikali ya Israel na mashambulizi ya kijeshi yaliyosababisha hasara kubwa katika nchi za Waislamu kwenye miaka ya hivi karibuni na kuwaambia vijana kwamba: Ninawataka nyinyi vijana, mjenge nguzo za kuamiliana kwa njia sahihi na kiungwana na ulimwengu wa Uislamu kwa msingi wa utambuzi sahihi, uoni mpana na kwa kutumia tajiriba chungu.
Barua kamili ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa nchi za Magharibi ni hii ifuatayo:
Matamshi yoyote kuhusu kubakishwa muundo wa vikwazo ni kinyume na makubaliano ya nyuklia
Matamshi yoyote kuhusu kubakishwa muundo wa vikwazo ni kinyume na makubaliano ya nyuklia
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amemtumia barua Rais Hassan Rouhani na ambaye pia ni Mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa akiashiria uchunguzi wa kina uliofanyika bungeni na katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 (JCPOA) na jinsi yalivyopita katika hatua zote za kisheria. Vilevile ametoa maagizo muhimu juu ya kulindwa maslahi ya kitaifa.
Matini kamili ya barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
Serikali ya Saudi Arabia inapaswa kubeba dhima kubwa ya tukio hilo chungu
Serikali ya Saudi Arabia inapaswa kubeba dhima kubwa ya tukio hilo chungu
Kufuatia maafa yaliyosababisha msiba mkubwa hii leo huko Mina, Saudi Arabia, ambapo idadi kubwa ya Wageni wa Mwenyezi Mungu wameaga dunia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe akieleza mshikamano wake na watu waliopatwa na msiba katika tukio hilo la kusikitisha na kutoa mkono wa taazia kwa familia zao. Vilevile Ayatullah Ali Khamenei ametangaza siku tatu za maombolezo ya taifa nchini Iran.
Siasa zilizojaa shari za Marekani na jinai za utawala wa Kizayuni vinapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza cha Waislamu
Siasa zilizojaa shari za Marekani na jinai za utawala wa Kizayuni vinapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza cha Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu akisema kuwa siasa zilizojaa shari za ubeberu za kuanzisha matatizo makubwa kwa Umma wa Kiislamu na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni na kuvunjiwa heshima Msikiti wa al Aqsa ndio suala lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa Waislamu wote. Ametoa wito kwa maulama na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kutekeleza majukumu yao mbele ya matukio hayo na kusema: Na Hija na mikusanyiko yake mikubwa ya Waislamu, ni mahala bora zaidi pa kujitokeza na kukabidhiana jukumu hilo la kihistoria, na fursa ya kujibari na kujitenga na washirikina ni mojawapo ya minasaba adhimu ya kisiasa inayopaswa kutumiwa vyema.
Ayatullah Khamenei ameashiria tukio la kusikitisha la kufariki dunia idadi kadhaa ya mahujaji ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka na majukumu makubwa ya kudhamini usalama wa Wageni wa Mwenyezi Mungu Rahmani na kusisitiza kuwa: Takwa letu kubwa ni kutekelezwa jukumu hilo.
Changanyeni elimu, kutafakari na ucha Mungu
Changanyeni elimu, kutafakari na ucha Mungu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma risala kwa kikao kikuu cha arubaini na tisa cha Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Ulaya na akiwanasihi vijana kwa kusema, ambatanisheni kazi ya kutafuta elimu na kutafakari, na yote hayo mawili yachanganyeni na ucha Mungu na kutakasa nafsi; wakati huo hakuna hazina itakayolingana na kuwa sawa na hiyo kwa nchi yenye utajiri wa vijana kama nyingi.

Anwani zilizochaguliwa