Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Fanyeni uchunguzi kuhusu Uislamu
Fanyeni uchunguzi kuhusu Uislamu
Kufuatia matukukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa na kuchapishwa kibonzo kinachovunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika jarida moja la Ufaransa na kushadidi wimbi la kuhujumu Uislamu la viongozi na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewaandikia ujumbe muhimu vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini. Ujumbe huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Hii hapa ni matini yake ya lugha ya Kiswahili:
Swala ni faradhi isiyo na kifani ya Kiislamu na nguzo ya dini na wenye dini
Swala ni faradhi isiyo na kifani ya Kiislamu na nguzo ya dini na wenye dini
Kikao cha 23 kikuu cha Swala nchini Iran kimefunguliwa leo asubuhi (Jumatano) kwa ujumbe wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Ahwaz (kusini magharibi mwa Iran).
Matini kamili ya ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambao umesomwa katika kikao hicho na Hujjatul Islam Walmuslimin Qarati, mkuu wa kamati ya kusimamisha Sala nchini Iran, ni kama ifuatavyo:
IRIB ina jukumu la kustawisha uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu
IRIB ina jukumu la kustawisha uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, ametoa hukumu ambayo ndani yake amemshukuru Mhandisi Izzatullah Zarghami, aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kutokana na jitihada zake kubwa mno na uchapaji kazi wake usiojua kuchoka na amemteua Bw. Mohammad Sarafraz kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Umoja wa Waislamu, Palestina na tofauti baina ya Uislamu sahihi na wa Kimarekani vipewe kipaumbele
Umoja wa Waislamu, Palestina na tofauti baina ya Uislamu sahihi na wa Kimarekani vipewe kipaumbele
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ametuma ujumbe muhimu kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu Alkaaba akisema kuwa suala la kuwaunganisha Waislamu na kuondoa tofauti baina yao ni jambo lililo na umuhimu mkubwa na kwamba Hija ni dhihirisho la umoja na udugu baina yao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Waislamu wanapokuwa kwenye Hija wanapasa kuzingatia mambo yanayowaunganisha na kuepuka yanayowatenganisha kwa sababu mikono miovu ya wakoloni tokea zamani imekuwa ikifanya njama za kuwatenganisha ili kudhamini maslahi yao haramu katika Umma wa Kiislamu.
Iran haitashirikiana na Marekani katika kadhia ya Daesh
Iran haitashirikiana na Marekani katika kadhia ya Daesh
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo ameruhusiwa kuondoka katika Hospitali ya Shahid Rajai mjini Tehran baada ya kukamilisha matibabu na kupata nafuu kikamilifu.
Kabla ya kuondoka hospitali hapo, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alifanyiwa mahojiano na mwandishi habari wa Shirika la Matangazo la Iran (IRIB) akieleza kuridhishwa na upasuaji na matibabu aliyopewa na akasema: “Ninarejea nyumbani nikiwa mzima wa afya ya mwili na mwenye nishati. Ninawashukuru wananchi kwa upendo wao walionionesha katika siku kadhaa zilizopita na ninaona haya na kujihisi mwenye deni zito kwa wananchi.”
Uchumi na utamaduni vinapaswa kupewa umuhimu
Uchumi na utamaduni vinapaswa kupewa umuhimu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameuita mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia ulioanza leo kuwa ni mwaka wa Uchumi na Utamaduni kwa Azma ya Taifa na Utendaji wa Kijihadi.
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia Ayatullah Khamenei amewapongeza Wairani wote dunia kwa mnasaba huo hususan familia za mashahidi na wanaopigana jihadi katika njia ya Uislamu.
Umoja wa Waislamu na kumtambua adui ndiyo dawa ya matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu
Umoja wa Waislamu na kumtambua adui ndiyo dawa ya matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe uliosomwa kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwenye uwanja wa Arafa mjini Makka akiitaja ibada ya Hija kuwa ni sikukuu kubwa ya Umma wa Kiislamu na fursa yenye muujiza unaoweza kutibu matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.
Ayatullah Khamenei ameashiria njama zinazofanywa na mabeberu wa kimataifa na kanali ya watenda jinai wa Kizayuni kwa ajili ya kuzima mwamko wa Kiislamu na kukwamisha masuala muhimu kama ukombozi wa Palestina na kusema umoja na udugu wa Kiislamu chini ya bendera ya tauhidi na kumjua adui na kukabiliana na njama zake ni miongoni mwa masomo muhimu ya ibada ya Hija na tiba mujarabu ya hali mbaya ya leo ya dunia ya Kiislamu. Ujumbe kamili wa Kiongozi Muadhamu kwa mahujaji ni huu ufuatao:
Mshindi halisi wa uchaguzi, ni taifa kubwa la Iran
Mshindi halisi wa uchaguzi, ni taifa kubwa la Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe muhimu wa kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa hamasa kubwa katika duru ya 11 ya uchaguzi wa kihistoria wa Rais wa Iran na duru ya 4 ya mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji.
Mwaka wa 1392 naupa jina la Mwaka wa Hamasa ya Kisiasa na Kiuchumi
Mwaka wa 1392 naupa jina la Mwaka wa Hamasa ya Kisiasa na Kiuchumi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa 1392 Hijria Shamsia akiashiria harakati ya maendeleo ya taifa la Iran katika mwaka uliopita hususan katika kukabiliana na ubeberu wa kimataifa katika nyanja za kiuchumi na kisiasa na kusema kuwa, mwaka wa 92 unatia matumaini na utaambatana na maendeleo, harakati na kuhudhuria kijihadi taifa la Iran katika nyanja za kisiasa na kichumi. Amesema: Kwa mtazamo huo mwaka huu mpya wa 1392 naupa jina la “Mwaka wa Hamasa ya Kisiasa na Kiuchumi”.
Vyombo vya habari na wasanii wanapaswa kutangaza jihadi kubwa ya wanawake wa Iran
Vyombo vya habari na wasanii wanapaswa kutangaza jihadi kubwa ya wanawake wa Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe katika kongamano la "Mashahidi Elfu Saba wa Kike" akiutaja mchango wa wanawake Waislamu wa Iran katika kuonesha kigezo bora na kipya kuwa ni wa kihistoria. Ameashiria kujitokeza wanawake wenye moyo wa Kikarbala katika harakati ya Mapinduzi ya Kiislamu na kujitetea kutakatifu na akasema kuwa, kumejitokeza uwezo na mvuto mpya katika zama za sasa kwa baraka ya damu ya wanawake hao ambao utakuwa na taathira katika hatima na nafasi ya wanawake duniani.
Imam Khamenei alishukuru taifa kwa ushujaa, kuona mbali na kutambua alama za nyakati
Imam Khamenei alishukuru taifa kwa ushujaa, kuona mbali na kutambua alama za nyakati
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumatatu amelipongeza taifa la Iran kutokana na kuona mbali, ushujaa na kutambua alama za nyakati kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman (10 Februari) ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, mahudhurio hayo makubwa ya wananchi ni tukio kubwa na adhimu.
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mahujaji
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mahujaji
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe muhimu kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu akiitaja ibada ya hija kuwa ni fursa adhimu ya kuchunguza njia za kurekebisha umma wa Kiislamu na masuala muhimu ya Ulimwengu wa Kiislamu. Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ni hii ifuatayo:
Mtuhumiwa wa kwanza katika jinai hii ni Wazayuni na serikali ya Marekani, waliofanya uovu huu wanapaswa kuadhibiwa
Mtuhumiwa wa kwanza katika jinai hii ni Wazayuni na serikali ya Marekani, waliofanya uovu huu wanapaswa kuadhibiwa
Kufuatia kitendo cha maadui wa Uislamu cha kumvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad (saw), Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa taifa la Iran na umma mkubwa wa Kiislamu akisema kuwa, siasa za kihasama za Wazayuni, Marekani na vinara wengine wa ubeberu wa kimataifa ndizo zilizohusika na harakati hiyo iliyojaa shari. Ameweka wazi sababu za kinyongo cha Wazayuni dhidi ya Uislamu na Qur’ani na akasisitiza kuwa, kama wanasiasa wa Marekani wanasema kweli katika madai yao kwamba hawakuhusika katika jinai hii, basi wanapaswa kuwapa adhabu inayonasibiana na jinai hii wale wote waliohusika na uhalifu huo mkubwa na waliowasaidia kifedha ambao wamezitia simanzi na maumivu nyoyo za mataifa ya Waislamu.
Swala inapaswa kuimarishwa katika jamii hususan kati ya vijana
Swala inapaswa kuimarishwa katika jamii hususan kati ya vijana
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye mkutano wa 21 wa taifa wa swala akisisitiza kuwa kuweka ibada hiyo katika nafasi yake inayostahiki kutatayarisha uwanja mzuri wa jamii kufikia kwenye kiwango kinachotakikana cha thamani za Uislamu. Amesema kuwa juhudi zote za masuala ya kiutamaduni, sanaa na elimu zinapaswa kufanyika na kutekelezwa kwa ajili ya kustawisha zaidi ibada ya swala kati ya wananchi hususan kizazi cha vijana.
Kiongozi Muadhamu amteua Sheikh Araki kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taqriib
Kiongozi Muadhamu amteua Sheikh Araki kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Taqriib
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amemteua Hujjatul Islam Walmuslimin Muhsin Araki kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu. Vilevile amemteuwa Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Ali Taskhiri kuwa mshauri wake mkuu katika masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.
Matini ya barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kumteuwa Sheikh Araki ni hii ifuatayo:

Anwani zilizochaguliwa