Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Uzalishaji wa Kitaifa, Kuunga Mkono Kazi na Rasilimali ya Kiirani”
Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Uzalishaji wa Kitaifa, Kuunga Mkono Kazi na Rasilimali ya Kiirani”
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe kwa taifa kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1391 Hijria Shamsia akitilia mkazo udharura wa kufanyika jihadi ya kiuchumi na kuwa na mahudhurio makubwa taifa la Iran katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Ameongeza kuwa sehemu muhimu ya jihadi ya kiuchumi inahusu suala la uzalishaji wa kitaifa na iwapo taifa litafanikiwa kutatua tatizo la uzalishaji wa ndani kwa kufanya hima, azma na kuwa macho sambamba na ratiba na mipango mizuri ya viongozi wa serikali, hapana shaka kwamba litashinda changamoto za adui.
Tutawaadhibu waliofanya jinai hiyo na washirika wao wa nyuma ya pazia
Tutawaadhibu waliofanya jinai hiyo na washirika wao wa nyuma ya pazia
Kufuatia mauaji ya kigaidi yaliyofaywa dhidi ya msomi kijana Shahid Ahmadi Roshan, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe muhimu akisema kuwa, kinyume na njama zinazofanywa na kambi ya ubeberu, taifa kubwa la Iran litadumisha njia ya maendeleo kwa nguvu na azma kubwa zaidi. Amesisitiza kuwa Iran itawaadhibu waliofanya jinai hiyo na washirika wao wa nyuma ya pazia.
Kufa shahidi ni taufiki ya Mwenyezi Mungu
Kufa shahidi ni taufiki ya Mwenyezi Mungu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema leo katika ujumbe uliotolewa kwa mnasaba wa kuwaenzi mashahidi wa Taasisi ya Jihadi ya Kujitosheleza ya jeshi la Sepah hususan Shahidi Brigedia Jenerali Hassan Muqaddam, kwamba matunda ya watu hawa wema yako katika mikono ya rijali wa jihadi, na watu waliolelewa katika mikono ya rijali hawa wana uwezo wa kudumisha njia yao yenye mwanga na nuru.
Umma wa Kiislamu unahitajia kusimama kidete na kuwa macho mbele ya hila za ubeberu
Umma wa Kiislamu unahitajia kusimama kidete na kuwa macho mbele ya hila za ubeberu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mnasaba wa mkusanyiko mkubwa wa ibada ya Hija akiyataja mapambano na mapinduzi yaliyofanyika katika baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa ni miongoni mwa masuala muhimu zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu na kwamba hakika zilizomo katika harakati na mapinduzi hayo ni aya na alama za wazi za Mwenyezi Mungu. Ayatullah Khamenei ameashiria wajibu mkubwa wa kizazi kilichoamka cha vijana, wasomi na maulamaa wa kidini katika kipindi muhimu sana cha sasa na akasisitiza kuwa: "Umma wa Kiislamu hususan mataifa yaliyoanzisha mapambano yanahitajia mambo mawili kwa ajili ya kudumisha njia hiyo nayo ni 'kuendelea kusimama kidete' na 'kuwa macho mbele ya hila za madola ya kibeberu ya kimataifa'.
Kiongozi Muadhamu atoa msaada kwa walioathiriwa na njaa Somalia
Kiongozi Muadhamu atoa msaada kwa walioathiriwa na njaa Somalia
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa msaada wa Riali milioni mia mbili kwa ajili ya watu walioathiriwa na baa la njaa nchini Somalia.
Fedha hizo zimewekwa katika akaunti nambari 99999 ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye Benki ya Melli nchini Iran.
Iran inalitambua suala la kupambana na ugaidi kuwa ni wajibu wake
Iran inalitambua suala la kupambana na ugaidi kuwa ni wajibu wake
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye mkutano wa Mapambano ya Dunia dhidi ya Ugaidi uliloanza leo mjini Tehran. Ayatullah Khemenei ameashiria katika ujumbe huo historia ya ugaidi wa madola makubwa ya kibeberu na uungaji mkono wao kwau tawala wa kigaidi na wa Kizayuni wa Israel na vilevile uovu wao mkubwa wa kusaidia kifedha na kirpopaganda ugaidi unaofanyika kwa mpangilio maalumu huku yakidai kupambana na ugaidi na akasema: Moja kati ya kazi muhimu za mkutano wa sasa ni kuainisha maana ya wazi na halisi ya ugaidi.
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu waelekea Madina kuwasilisha rambirambi
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu waelekea Madina kuwasilisha rambirambi
Wawakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wameelekea katika mji mtakatifu wa Madina kuwasilisha salamu za rambirambi za Kiongozi Muadhamu kufuatia kifo cha Allamah Sheikh Muhammad Ali al Amri ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia.
Taarifa ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu kuwashukuru wananchi wa Qum
Taarifa ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu kuwashukuru wananchi wa Qum
Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mwishoni mwa safari ya siku kumi ya Ayatullah Ali Khamenei katika mji mtakatifu wa Qum imetoa shukrani za dhati kwa matabaka mbalimbali ya wananchi waumini, wenye maarifa na wakarimu na hamasa kubwa iliyoonyeshwa na wananchi wa Qum. Ofisi hiyo pia imewashukuru maraji', maulamaa na wanafunzi wa mji huo na kuelezea matumaini yake kwamba safari ya Kiongozi Muadhamu mjini humo itafungua ukurasa mpya katika historia iliyojaa fahari ya Qum.
Mahudhurio ya vijana yanapaswa kutia nishati na kuhuisha misikiti
Mahudhurio ya vijana yanapaswa kutia nishati na kuhuisha misikiti
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye kikao cha 19 taifa cha swala akisema kuwa ibada ya swala ni dhihirisho la mchanganyiko wa dunia na akhera na mfungamano wa mtu binafsi na jamii. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa misikiti katika kila eneo na kitongoji inapaswa kuwa makimbilio ya amani, kheri na baraka, shule ya tafsiri ya Qur'ani na hadithi, minbari ya maarifa ya kijamii na kisiasa na kituo cha mawaidha na malezi ya maadili bora.
Serikali ya Marekani inapaswa kuwaadhibu ipasavyo wahusika wakuu wa jinai hii kubwa
Serikali ya Marekani inapaswa kuwaadhibu ipasavyo wahusika wakuu wa jinai hii kubwa
Kufuatia kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur’ani nchini Marekani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe muhimu kwa taifa la Iran na umma mkubwa wa Kiislamu akitaja makundi ya Kizayuni ndani ya serikali ya Marekani kuwa ndiyo yaliyopanga njama hiyo ya kuchukiza. Ayatullah Khamenei amebainisha malengo ya siri ya chuki za Wazayuni dhidi ya Uislamu na Qur’ani akisisitiza kuwa: “Ili kuthibitisha madai yake kwamba haikuhusika katika njama hiyo, serikali ya Marekani inawajibika kuwaadhibu ipasavyo wahusika wakuu na watekelezaji wake.” Matini kamili ya ujumbe wa Walii amri wa Waislamu duniani ni hii ifuatayo:
Tuwasaidie haraka ndugu zetu waliopatwa na masaibu wa Pakistan kwa msingi wa udugu wa Kiislamu
Tuwasaidie haraka ndugu zetu waliopatwa na masaibu wa Pakistan kwa msingi wa udugu wa Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewatumia ujumbe Waislamu kote duniani akiashiria maafa makubwa ya mafuriko yaliyotokea nchini Pakistan, kiwango kikubwa cha hasara iliyosababishwa na mafuriko hayo na haja ya misaada ya dharura ya mamilioni ya Waislamu wa Pakistan. Amesisitiza kuwa: “Katika kipindi hiki nyeti tunapaswa kutekeleza wajibu wetu kwa mujibu wa udugu wa Kiislamu na kuwasaidia haraka ndugu zetu waliopatwa na masaibu."
Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Waislamu kote ulimwenguni ni hii ifuatayo:
Taasisi zote husika zinapaswa kuwapa wafitini jaza yao kwa uhalifu waliotenda
Taasisi zote husika zinapaswa kuwapa wafitini jaza yao kwa uhalifu waliotenda
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kutimia siku ya saba tangu kuuawa shahidi makumi ya wananchi waumini wa mji wa Zahedan huko kusini mashariki mwa Iran katika milipuko ya kigaidi iliyolenga msikiti mkuu wa mji huo akivitaja vyombo vya ujasusi vya Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Uingereza kuwa ndio wahusika wakuu wa jinai hiyo. Ayatullah Khamenei amesema kuwa moja ya malengo makuu ya maadui katika kutekeleza shambulio hilo la kigaidi ni kuzusha hitilafu na fitina za kimadhehebu lakini Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu mikono ya ubeberu wa kimataifa kufikia lengo lake. Vilevile amevitaka vyombo vyote husika vya Serikali, Bunge na Mahakama kupambana vilivyo na maadui wa umoja na usalama wa taifa na kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.
Jinai ya baharini ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni dalili ya kuchanganyikiwa utawala huo ghasibu
Jinai ya baharini ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni dalili ya kuchanganyikiwa utawala huo ghasibu
Kufuatia jinai na shambulizi la kinyama lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msafara wa Uhuru uliokuwa umebeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wananchi wa Ukanda wa Gaza, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe akiitaja jinai hiyo kuwa ni shambulizi dhidi ya ubinadamu kote duniani. Ayatullah Khamenei amesema: "Leo hii Palestina si suala la Waarabu au hata Waislamu pekee, bali ni kadhia inayohusu haki za binadamu za dunia ya sasa, na waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel hususan Marekani, Uingereza na Ufaransa wanapaswa kuwajibika vilivyo katika suala hilo."
Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni hii ifuatayo:
Mwaka huu ninauita mwaka wa
Mwaka huu ninauita mwaka wa "Hima Zaidi na Kazi Zaidi
«يا مقلّب القلوب و الأبصار. يا مدبّر اللّيل و النّهار» Ewe Mola unayebadilisha nyoyo na macho ya watu. Ewe Mola unayeendesha usiku na mchana. «يا محوّل الحول و الأحوال» Ewe Mola unayebadilisha miaka na hali. «حوّل حالنا الى احسن الحال» Badili hali zetu na uzifanye bora zaidi.
Taifa la Iran Limechukua Uamuzi wa Kufikia Kilele cha Maendeleo na Ufanisi
Taifa la Iran Limechukua Uamuzi wa Kufikia Kilele cha Maendeleo na Ufanisi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe akiwashukuru wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: "Marafiki na maadui wanapaswa kuelewa kwamba taifa la Iran limetambua njia yake na kuchukua uamuzi wa kufikia kilele cha maendeleo na ufanisi na litaondoa vizuizi vya aina yoyote katika njia hiyo."
Ujumbe kamili wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni huu ufuatao:

Anwani zilizochaguliwa