Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mahujaji mwaka 1430
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mahujaji mwaka 1430
Bismillahi Rahmani Rahiim
Msimu wa Hija ni machipuo ya umaanawi na kung'ara kwa tauhidi katika upeo wa dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile.
Kipindi cha Uongozi wa Bwana Zarghami Chaongezwa kwa Miaka Mingine Mitano
Kipindi cha Uongozi wa Bwana Zarghami Chaongezwa kwa Miaka Mingine Mitano
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza muda wa kuhudumu Sayyid Ezzatollah Zarghami kama Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB. Katika ujumbe wake uliotolewa Jumamosi, Ayatullahil Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya kutumiwa mafanikio ya sasa ya shirika la IRIB na hima kubwa kwa ajili ya kuondoa nakisi na mapungufu yaliyopo na kukifikisha chombo hicho cha kiutamaduni katika daraja ya chombo cha habari ambacho dini maadili mema, matumaini na kuelimisha jamii vitakuwa madhihirisho yake makuu.
Ijazeni Miskiti kwa Harakati na Nishati Kama Zilivyo Nyoyo za Vijana
Ijazeni Miskiti kwa Harakati na Nishati Kama Zilivyo Nyoyo za Vijana
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei amesema katika ujumbe wake uliosomwa kwenye Mkutano wa 18 wa Taifa wa Swala kwamba kuupa mkutano wa mwaka huu jina la vijana ni hatua inayostahili pongezi. Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa kuwaelimisha vijana kuhusu usafi na raha ya Swala ni huduma kubwa mno kwao na kwa mustakbali utakaojengwa kwa hima ya vijana hao.
Mashahidi ni Dhihirisho la Kipindi Chenye Thamani Kubwa cha Kujilinda Kutakatifu
Mashahidi ni Dhihirisho la Kipindi Chenye Thamani Kubwa cha Kujilinda Kutakatifu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mnasaba wa siku ya kuadhimisha na kuwaenzi mashahidi na wale waliojitolea katika kipindi cha miaka 8 ya kujilinda kutakatifu akisema kuwa mashahidi ni dhihirisho na vinara wa kipindi hicho cha thamani kubwa. Ayatullah Khamenei amesema kuwa kuwaenzi mashahidi azizi na wenye daraja ya juu ambao walidhihirisha johari inayong'ara ya taifa lenye imani la Iran kwa kusabilia nafsi zao, kunaleta uhai mpya.
Wananchi Azizi wa Kurdistan Wanapaswa Kuwatambua Vizuri Maadui Zao
Wananchi Azizi wa Kurdistan Wanapaswa Kuwatambua Vizuri Maadui Zao
Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi na pongezi kwa wananchi kufuatia tukio la mauaji ya kigaidi la kuuawa shahidi Mamusta Sheikhul Islam, mwakilishi wa wananchi wa mkoa wa Kurdistan katika Baraza la Wataalamu wa Kumchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Matini ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ni hii ifuatayo:
Rais Aliyechaguliwa ni Rais wa Jamhuri na Taifa Zima la Iran
Rais Aliyechaguliwa ni Rais wa Jamhuri na Taifa Zima la Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ametoa ujumbe muhimu akitaja mahudhurio makubwa, ya kishindo na yaliyotawaliwa na utulivu ya taifa kubwa la Iran katika Ijumaa ya hamasa ya tarehe 12 Juni kuwa ni rehma ya Mola Mwenye hikima na tukio la kustaajabisha lisilokuwa na kifani.
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa sikukuu ya Nairuzi mwaka 1388
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa sikukuu ya Nairuzi mwaka 1388
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe wa mwaka mpya wa 1388 Hijria Shamsia akiutaja mwaka huo kuwa ni muhimu na akaelezea matumaini ya nguvu ya imani ya taifa la Iran kushinda na kupata mafanikio katika mwaka huu. Ayatullah Khamenei amesema: "Kwa kuzingatia umuhimu mkubwa na wa kimsingi wa kuwa na tadbiri na busara katika kutumia rasilimali za nchi, mwaka mpya ninaupa jina la mwaka wa Marekebisho ya Kigezo cha Matumizi katika Nyanja na Mambo yote."
Kikao cha Kimataifa cha Kuwaunga Mkono Wananchi Wapalestina
Kikao cha Kimataifa cha Kuwaunga Mkono Wananchi Wapalestina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jinai zilizofanywa na Wazayuni wahalifu katika tukio la kihistoria la Ghaza zimethibitisha kuwa, kiu ya kufanya ukatili na jinai waliyo nayo viongozi wa utawala pandikizi wa Kizayuni haitofautiani hata chembe na kiu waliyokuwa nayo viongozi wa utawala huo katika miongo ya mwanzoni mwa maafa ya Ghaza.

Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema hayo Jumatano Machi 4, 2009 katika kongamano la kimataifa la "Palestina Dhihirisho la Istikama; Ghaza Muhanga wa Jinai" linalofanyika mjini Tehran na kuongeza kuwa, kuna matukio muhimu na ya maana sana yametokea na kuweka wazi zaidi upeo wa siku za usoni wa kadhia ya Palestina sambamba na kubainisha majukumu yetu kuhusu kadhia hiyo ambayo bado ni suala kuu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Anwani zilizochaguliwa