Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Kuna ulazima wa kuundwa kamati ya kuchunguza tukio la Mina
Kuna ulazima wa kuundwa kamati ya kuchunguza tukio la Mina
Ayatullah Khamenei ameashiria tukio la kusikitisha la Mina huko Saudi Arabia na kusema tukio hilo ni msiba halisi kwa taifa la Iran kutokana na kufariki dunia maelfu ya mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu hususan mamia ya mahujaji wa Kiirani. Ameashiria udharura wa kuundwa kamati ya kutafuta ukweli kuhusu tukio hilo itakayoshirikisha nchi za Kiislamu ikiwemo Iran na kusema: Serikali ya Saudi Arabia haitekelezi majukumu yake katika suala la kusafirisha miili mitoharifu ya mahujaji wa Iran waliofariki dunia na hadi sasa Jamhuri ya Kiislamu imelinda heshima ya udugu katika ulimwengu wa Kiislamu kwa kuonesha uvumilivu na adabu ya Kiislamu; lakini pia wanapaswa kutambuwa kwamba, utovu wa heshima wa aina yoyote ile kwa makumi ya maelfu ya mahujaji wa Iran walioko Makka na Madina na kutotekeleza majukumu yao kwa ajili ya kusafirisha miili mitoharifu ya mahujaji wa Iran kutakabiliwa na jibu kali na la kuumiza.
Siasa zetu za kukabiliana na ubeberu wa Marekani kamwe hazitabadilika
Siasa zetu za kukabiliana na ubeberu wa Marekani kamwe hazitabadilika
Wananchi wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na wenye imani na umoja wa Iran leo wamefanya sijda za shukrani katika pembe zote za nchi hii yenye fahari, kwa ajili ya kumshukuru Mola wao kwa kuwawezesha kufunga, kufanya ibada na kujitakasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Huku wakiwa kwenye swala ya Idul- Fitr wamemwomba Mwenyezi Mungu wao Mkarimu awawezeshe kudumu kwenye wongofu na saada ya humu duniani na huko Akhera. Katika kitovu cha fahari hii ya kihistoria, wananchi wakazi wa mji mkuu Tehran, wameswali Swala ya Idi kwa uimamu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika uwanja wa Muswala wa mjini Tehran.
Qarii wa Qur’ani anapaswa kuwa na imani ya kweli ya maana ya aya za kitabu hicho
Qarii wa Qur’ani anapaswa kuwa na imani ya kweli ya maana ya aya za kitabu hicho
Katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao imeshushwa ndani yake Qur'ani, alasiri ya leo (Alkhamisi) kumefanyika mahafali ya Qiraa ya Qur'ani Tukufu hapa mjini Tehran yaliyohudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika mahafali hayo yaliyojaa nuru na kuhinikiza manukato na umaanawi wa Qur'ani, maqari na mahafidh 15 wa Qur'ani Tukufu pamoja na wahadhiri wa Qur'ani kutoka kona zote za Iran, wamesoma baadhi ya aya tukufu za maneno hayo ya Mwenyezi Mungu.
Dunia nzima inapaswa kuwasaidia kwa silaha wananchi wa Palestina
Dunia nzima inapaswa kuwasaidia kwa silaha wananchi wa Palestina
Mvuto wa sikukuu ya Idul Fitr umeongezeka maradufu leo kutokana na kuswaliwa Swala ya Idi katika kila kona ya Iran ya Kiislamu huku wananchi waumini wenye mshikamano thabiti wa Iran wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye misikiti na maeneo mbalimbali ili kutekeleza ibada hiyo tukufu wakimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa taufiki ya kutimiza mwezi wa taqwa na ibada, mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika ibada hiyo ya kimaanawi ambayo kitaifa imesaliwa katika eneo la "Muswala" wa Tehran, Waislamu wa Tehran wamejumuika kwa wingi kwenye eneo hilo mapema leo asubuhi na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa swala hiyo iliyongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ninaunga mkono harakati za kidiplomasia za serikali
Ninaunga mkono harakati za kidiplomasia za serikali
Sherehe ya kuapishwa na kupewa vyeo wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu vya maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanyika mapema leo ikihudhuriwa na Amiri jeshi Mkuu wa majeshi yote Ayatullah Ali Khamenei katika Chuo Kikuu cha Jeshi la Anga cha Shahid Sattari.
Amiri Jeshi Mkuu wa Iran ameashiria vitisho vya kukirihisha vinavyotolewa mara kwa mara na maadui wa taifa la Iran na kusema: "Watu wote wenye tabia ya kutoa vitisho vya maneno dhidi ya Iran wanapaswa kuelewa kwamba, jibu letu kwa chokochoko za aina yoyote litakuwa kali na zito."
Wazayuni wanafurahishwa na hali mbaya ya Misri, Iraq na nchi nyingine za Kiislamu zilizokumbwa na hitilafu
Wazayuni wanafurahishwa na hali mbaya ya Misri, Iraq na nchi nyingine za Kiislamu zilizokumbwa na hitilafu
Taifa la waumini na lenye umoja na mshikamano la Iran leo limeshiriki kwa wingi katika Swala ya Idil Fitri kote nchini na kumshukuru Mwenyezi Mungu SW kwa kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mjini Tehran Swala ya Idi iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu imeongozwa na Ayatullah Imam Ali Khamenei katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran na kilomita kadhaa katika mitaa ya kandokando yake.
Imani thabiti ya Imam Khomeini kwa Mwenyezi Mungu, kwa wananchi na kwake yeye mwenyewe iliandaa uwanja wa kupatikana ushindi na maendeleo ya kupigiwa mfano taifa la Iran
Imani thabiti ya Imam Khomeini kwa Mwenyezi Mungu, kwa wananchi na kwake yeye mwenyewe iliandaa uwanja wa kupatikana ushindi na maendeleo ya kupigiwa mfano taifa la Iran
Idadi kubwa isiyo na kifani ya wananchi waumini na wanapinduzi kutoka kila pembe ya Iran, leo wamekutanika kwenye mkusanyiko adhimu na uliojaa hamasa katika Haram toharifu ya Imam Khomeini (MA) mjini Tehran na kwa mara nyingine kutangaza utiifu wao kwa kipenzi chao huyo aliyetangulia mbele ya Haki, Imam Khomeini (MA) ambaye ni kamba madhubuti ya umoja na utukufu wa taifa na viongozi wa Iran.
Kuna watu wanajifanya kutoa maoni kuhusu uchaguzi wa Iran wakati watu hao hao wanafanya jinai kwenye jela ya Guantanamo
Kuna watu wanajifanya kutoa maoni kuhusu uchaguzi wa Iran wakati watu hao hao wanafanya jinai kwenye jela ya Guantanamo
Leo asubuhi (Jumatatu) kumefanyika sherehe za kuhitimu mafunzo wanachuo wa Chuo Kikuu cha malezi na maafisa wa kijeshi cha cha Imam Hussein AS zilizohudhuriwa na Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sherehe hizo zimefanyika sambamba na siku za maadhimisho ya ukombozi wa Khorramshahr.
Taifa la Iran halijawahi kumchokozi yeyote lakini halitanyamazia kimya uchokozi wa aina yoyote
Taifa la Iran halijawahi kumchokozi yeyote lakini halitanyamazia kimya uchokozi wa aina yoyote
Mapema leo Ayatullah Ali Khamenei ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran amekagua gwaride la vikosi vya jeshi na jeshi la kujitolea na Basij katika mkoa wa Khorasani Kaskazini katika kambi ya Shahid Nuri ya Kikosi cha nchi kavu cha Jawadul Aimma cha jeshi la Sepah huko Bojnurd.
Baada ya kuwasili katika kambi hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikwenda moja kwa moja kwenye makaburi ya kumbukumbu ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuwasomea al Fatiha sambamba na kuwaombea dua mashahidi hao.
Kubakia nyuma kwa maadui wa Uislamu mbele ya taifa la Iran na mwamko wa Kiislamu ndiyo sababu iliyowafanya wamvunjie heshima Mtume (saw)
Kubakia nyuma kwa maadui wa Uislamu mbele ya taifa la Iran na mwamko wa Kiislamu ndiyo sababu iliyowafanya wamvunjie heshima Mtume (saw)
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amekagua gwaride na sherehe za kuapishwa na kupewa vyeo wanafunzi wa vyuo vikuu vya maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu. Ametoa hotuba katika hadhara ya jeshi hilo akiashiria jinai ya kumvunjia heshima Mtukufu Mtume Muhammad (saw) na kusema kuwa, mataifa mbalimbali yanayoelewa siasa za kuuhujumu Uislamu za ubeberu na Uzayuni yanaelekeza kidole cha tuhuma kwa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, na viongozi wa nchi hizo wanapaswa kuzuia hatua kama hizo za kiendawazimu na kuthibitisha kwamba hawakushiriki katika jinai hiyo kubwa.
Mabadiliko ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu yanaainisha mustakbali
Mabadiliko ya sasa ya ulimwengu wa Kiislamu yanaainisha mustakbali
Siku ya leo ya Idul Fitr, idi ya wampwekeshao Mwenyezi Mungu, Iran imeghiriki katika nuru na uja huku wananchi wa jiji la Tehran wakishiriki kwa wingi katika ibada ya swala ya Idi iliyoongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
Katika hotuba za swala ya Idi, Ayatullah Khamenei ameyataja matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu kuwa ni ya kushangaza na yasiyo na kifani. Amesema kuwa, matukio hayo ambayo yanaainisha njia ya mustakbali wa ulimwengu wa Kiislamu yataendelea kwa kasi na mwenendo huo huo kwa baraza zake Mwenyezi Mungu.

Anwani zilizochaguliwa