Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Siku ya Quds ni kumbukumbu kubwa zaidi ya marehemu Imam Khomeini (M.A)
Siku ya Quds ni kumbukumbu kubwa zaidi ya marehemu Imam Khomeini (M.A)
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameongoza swala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran ambako alihutubia umati mkubwa wa hadhirina akibainisha mwenendo wa kisiasa wa Bwana wa Wachamungu Ali Bin Abi Twalib (as) na kusema kuwa sera za kisiasa za Imam khomeini zinaoana na mwenendo na sira ya Amirul Muuminin. Ayatullah Ali Khamenei amesisitizia kuwa kwa uwezo wake Allah, taifa kubwa la Iran Ijumaa ijayo litaungana na kuongoza mataifa yanayopambana dhidi ya dhulma duniani kwa kubeba bendera ya kuwateta wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
Kuweni Thabiti na Shadidi kwa Maadui na Wenye Huruma na Upole kwa Marafiki
Kuweni Thabiti na Shadidi kwa Maadui na Wenye Huruma na Upole kwa Marafiki
Wasomaji bora wa Qur'ani, walimu na mahafadhi wa kitabu hicho kitukufu wamekutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei katika Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran kwa mnsaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa rehma na msimu wa machipuo wa Qur'ani. Kikao hicho kilichodumu kwa masaa matatu kilitiwa nuru kwa kisomo cha aya za Qur'ani Tukufu cha makurai na kutumbuizwa kwa qasida za kumsifu Mtume Muhammad (saw).
Rais na Serikali Mpya ni ya Wananchi Wote wa Irani
Rais na Serikali Mpya ni ya Wananchi Wote wa Irani
Sherehe za kumuidhinisha Dakta Mahmoud Ahmadinejad kuwa Rais wa kumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimefanyika leo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa mwokozi aliyeahidiwa Imam wa zama Mahdi (as). Katika sherehe hizo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapongeza wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 12 Juni hapa nchini na kumuidhinisha rasmi Dakta Mahmoud Ahmadinejad kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu.
Uchaguzi wa Rais wa Tarehe 12 Juni ni Dhihirisho la Imani ya Taifa kwa Mfumo wa Kiislamu
Uchaguzi wa Rais wa Tarehe 12 Juni ni Dhihirisho la Imani ya Taifa kwa Mfumo wa Kiislamu
Swala ya Ijumaa ya leo mjin Tehran imeongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei. Kiongozi Muadhamu ametoa hotuba muhimu na ya kihistoria katika swala hiyo akisisitiza kuwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kutaka msaada wake na utulivu wa moyo ni miongoni mwa mambo yaliyolisaidia taifa la Iran kuvuka tufani na mawimbi makubwa ya kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Ayatullah Khamenei amezungumzia pia mwenendo wa uchaguzi wa Rais uliofanyika siku chache zilizopita hapa nchini na masuala yaliyojitokeza baada ya uchaguzi na akasema: "Mahudhurio makubwa na yasiyokuwa na kifani ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa Rais wa tarehe 12 Juni na kujiamini kwa taifa kubwa la Iran katika siku hiyo ilikuwa zilzala na mtetemeko mkubwa wa kisiasa kwa maadui na sherehe ya kihistoria ya wapenzi wa Iran na Mapinduzi ya Kiislamu.
Taifa la Iran linakuona kusimama kidete mbele ya madhalimu kuwa ni katika fahari na thamani zake kuu
Taifa la Iran linakuona kusimama kidete mbele ya madhalimu kuwa ni katika fahari na thamani zake kuu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi amesema katika sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa mbora wa wanawake duniani Bibi Fatima al Zahra (as) na Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) kwamba uchaguzi wa Rais uliofanyika Ijumaa iliyopita nchini Iran ni muujiza wa Mwenyezi Mungu. Ayatullah Khamenei ameashiria mahudhurio makubwa ya wananchi katika uchaguzi huo na akasema: Taifa lenye mwamko, pevu na lililo macho la Iran limeonyesha katika zoezi hilo kwamba lingali linafungamana na maneno, njia na malengo yaliyoainishwa na Imam Khomeini na linatafuta ufanisi na maendeleo yake katika njia hiyo.
Kiongozi Muadhamu akagua vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mkoani Kurdistan
Kiongozi Muadhamu akagua vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mkoani Kurdistan
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kulinda usalama na kuleta utulivu katika maisha ya wananchi ndiyo falsafa ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba kuendelea kujiimarisha na kuweko tayari kitaifa hususan miongoni mwa vikosi vya ulinzi, ndiyo mambo makuu yanayoweza kulinda heshima na utukufu wa taifa la Iran.
Sala ya Idil Fitri Yasalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Sala ya Idil Fitri Yasalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Wananchi waumini na wampwekeshao Mwenyezi Mungu wa Iran wameipa Saumu na ibada walizotekeleza katika mwezi mzima wa Ramadhani sura ya sherehe ya kitaifa ya kiibada na kimaanawi kutokana na kuhudhuria kwa wingi mno katika Sala ya Idi iliyosaliwa asubuhi ya leo katika uwanja mkuu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran. Katika anga iliyotawaliwa na hali ya uchangamfu maalumu wa kimaanawi uwanja mkuu wa Sala ya Ijumaa ulifurika umati mkubwa wa waumini ambao walishiriki katika Sala ya Idil Fitri iliyosalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Khamenei.
Maadhimisho ya 19 ya Kukumbuka Kufariki Dunia Imam Khomeini
Maadhimisho ya 19 ya Kukumbuka Kufariki Dunia Imam Khomeini
Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mkusanyiko wa mamilioni ya watu waliojumuika Jumanne Juni 3, 2008 katika Haram ya Imam Khiomeini (quddisa sirruh) kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 19 wa kufariki dunia shakhsia huyo mkubwa wa zama hizi kwamba Mapinduzi ya Kiislamu kama alivyosema Imam Khomeini, ni mali ya matabaka na vizazi vya sasa na vijavyo vya Iran na kwamba taifa hili kubwa litalinda amana hiyo kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kutekeleza wasia na miongozo ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) na kulinda kaulimbiu, misimamo na matukufu ya kimsingi ya Mapinduzi, sambamba na kuzingatia maendeleo, ubunifu na kulinda heshima.

Anwani zilizochaguliwa