Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Kiongozi Muadhamu apiga kura mapema asubuhi
Kiongozi Muadhamu apiga kura mapema asubuhi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi yaa Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo katika dakika za mwanzoni mwa uchaguzi wa 9 wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amehudhuria katika kituo cha kupigia kura katika Husainiya ya Imam Khomeini na kutumbukiza kura yake katika sanduku la kupigia kura.
Baada ya kupiga kura, Ayatullah Khamenei amesema uchaguzi wa 9 wa Bunge hapa nchini una umuhimu mkubwa katika pande mbalimbali. Amewausia wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura na kutekeleza wajibu huo muhimu mapema kwa nia ya ikhlasi ili amali yao hiyo ipate baraka zaidi za Mwenyezi Mungu.
Iran italisaidia taifa lolote litakalosimama kupambana na utawala ghasibu wa Israel
Iran italisaidia taifa lolote litakalosimama kupambana na utawala ghasibu wa Israel
Sambamba na siku hizi za kuadhimisha mwaka wa 33 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khameni leo amehutubia Swala ya Ijumaa mjini Tehran akitoa uchambuzi kamili kuhusu matunda na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuzungumzia masuala muhimu ya ndani, vitisho vya maadui na hali ya kieneo na kimataifa na vilevile uchaguzi ujao wa Bunge la 9 la Iran.
Jeshi la Iran litajibu uchokozi wa aina yoyote kwa ngumi ya chuma
Jeshi la Iran litajibu uchokozi wa aina yoyote kwa ngumi ya chuma
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amehutubia sherehe za kuapishwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Chuo Kikuu cha maafisa wa jeshi cha Imam Ali (as) na kusema kuwa jeshi la Iran ni dhihirisho la izza na nguvu ya taifa na nchi na ngao imara ya ulinzi wa taifa. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa maadui hususan Marekani, vibaraka wake na utawala wa Kizayuni wa Israel wanapaswa kuelewa kwamba taifa la Iran halitashambulia nchi na taifa lolote lakini litajibu mashambulizi na hata vitisho kwa nguvu zote kwa njia ambayo itawasambaratisha kwa ndani wachokozi na wavamizi.
Siasa za ubeberu za kueneza hofu kuhusu Iran katika Mashariki ya Kati hazitazaa matunda
Siasa za ubeberu za kueneza hofu kuhusu Iran katika Mashariki ya Kati hazitazaa matunda
Alaasiri ya leo vikosi vya jeshi na polisi ya Iran katika mkoa wa Kermanshah vilifanya gwaride lililohudhuriwa na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran Ayatullah Ali Khamenei.
Baada ya kuwasili katika kituo cha kikosi cha 81 cha jeshi, Amiri Jeshi Mkuu alielekea moja kwa moja katika mnara wa kumbukumbu ya mashahidi wa vita na kuwakumbuka kwa kuwasomea al Fatiha na kuwaombea rehma na maghufira na daraja za juu peponi.
Hapana shaka kwamba Palestina itarejea katika mikono ya Uislamu
Hapana shaka kwamba Palestina itarejea katika mikono ya Uislamu
Katika shughuli ya kumbukumbu ya mwaka wa 22 tangu Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu afariki dunia, hii leo wananchi wa Iran ya Kiislamu wameifanya haram ya shakhsia huyo kuwa medani ya kudhihirisha uaminifu wao mkubwa kwa njia na fikra za kiongozi huyo. Maelfu ya wananchi hao wamedhihirisha hisia zao za upendo na mahaba kwa hayati Imam Khomeini na kutangaza tena baia’ na utiifu wao kwa khalifa wa kiongozi wa baada yake, Ayatullah Ali Khamenei.
Kushindwa siasa za Marekani Mashariki ya Kati ni ishara ya kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu
Kushindwa siasa za Marekani Mashariki ya Kati ni ishara ya kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuwa kushindwa siasa za Marekani Mashariki ya Kati ni kielelezo cha kutimia baadhi ya ahadi za Mwenyezi Mungu kwa Taifa la Iran.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo leo wakati wa kukagua gwaride la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Maafisa wa Jeshi cha Imam Hussein mjini Tehran na kuongeza kuwa kushindwa kwa siasa za Shetani Mkubwa yaani Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kuhuishwa nara zinazotoa bishara njema za Kiislamu baina ya mataifa mbalimbali ni kielelezo cha kutimia sehemu moja ya ahadi za Mwenyezi Mungu kwa taifa la Iran.
Msitosheke na mpaka maalumu katika harakati ya maendeleo
Msitosheke na mpaka maalumu katika harakati ya maendeleo
Sherehe za nne za wanachuo na kuhitimu wanafunzi wa vyuo vikuu vya maafisa wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimefanyika leo katika Chuo Kikuu cha Jeshi la Anga cha Shahid Sattari zikihudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
Mwanzoni mwa sherehe hizo Amiri jeshi wa majeshi ya Iran alikwenda kwenye kumbukumbu ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa ajili ya kuwasomea al Fatiha na kuwaombea dua na daraja za juu peponi. Baada ya hapo Ayatullah Khamenei alikagua gwaride la vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu.
Taifa la Palestina litakunja jamvi la utawala bandia wa Kizayuni
Taifa la Palestina litakunja jamvi la utawala bandia wa Kizayuni
Iran ya Kiislamu leo katika sikukuu ya Idul Fitr ilighiriki katika nuru, dua na ibada. Baada ya kukamilisha mwezi mmoja wa ibada ya funga, taifa la waumini la Iran limemuomba na kumtaradhia Mola Mlezi alipe idi ya kheri na mema ya Mtume Muhammad (saw) na Ali zake watukufu.
Swala ya Idul Fitr mjini Tehran iliongozwa na Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika hotuba za swala hiyo Ayatullah Khamenei ametoa mkono wa idi kwa umma wa Kiislamu hususan taifa azizi la Iran akisema kuwa kuelewa vyema matukufu ya mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa neema kubwa. Amewausia Waislamu wote kutambua thamani ya neema hiyo ya Mwenyezi Mungu na kulinda matunda ya thamani na ghali ya kiroho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Imam Khomeini na sera zake ndio kielelezo kikubwa zaidi cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
Imam Khomeini na sera zake ndio kielelezo kikubwa zaidi cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
Taifa lenye uaminifu, kakamavu na erevu la Iran leo limeshiriki kwa wingi katika shughuli ya kukumbuka mwaka wa 21 tangu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Ruhullah Khomeini afariki dunia na kutoa tena mkono wa utiifu kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei. Hadhara hiyo kubwa iliyokusanyika katika ziara la Imam imehutubiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye amemtaja Imam Khomeini kuwa ndiyo nembo kubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.
Kusimama kidete taifa la Iran kumeimarisha zaidi mfumo wa Kiislamu
Kusimama kidete taifa la Iran kumeimarisha zaidi mfumo wa Kiislamu
Sherehe ya kuhitimu masomo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Imam Hussein (as) zimefanyika leo tarehe 3 Khordad (24 Mei) sambamba na maadhimisho ya siku ya kukombolewa mji wa Khorramshahr wa kusini mwa Iran kutoka mikononi mwa wavamizi wa utawala wa Saddam Hussein wa Iraq. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
Ayatullah Khamenei ambaye pia ndiye Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametembelea pia makaburi ya mashahidi na kuwasomea al Fatiha na dua. Baada ya hapo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekagua paredi ya maafisa wa kijeshi waliokuweko hapo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ameshiriki katika marasimu ya maombolezo na kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Mbora wa wanawake wote duniani Bibi Fatima al Zahara (as) yaliyofanyika katika Huseiniya ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ameshiriki katika marasimu ya maombolezo na kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Mbora wa wanawake wote duniani Bibi Fatima al Zahara (as) yaliyofanyika katika Huseiniya ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ameshiriki katika marasimu ya maombolezo na kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Mbora wa wanawake wote duniani Bibi Fatima al Zahara (as) yaliyofanyika katika Huseiniya ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu.
Majlisi hiyo ambayo imehudhuriwa pia na maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali ya wananchi na viongozi wa ngazi za juu serikalini itaendelea hadi siku ya Jumanne ya tarehe 17 May.
Mfumo wa Kiislamu umeleta mwamko wa Kiislamu na kuwakasirisha mabeberu hususan Marekani
Mfumo wa Kiislamu umeleta mwamko wa Kiislamu na kuwakasirisha mabeberu hususan Marekani
Meli ya Kijeshi ya "Jamaran" ambayo ni ya kwanza kutengenezwa na wataalamu wa jeshi la wanamaji na wataalamu vijana wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezinduliwa leo na Amiri Jeshi wa majeshi yote ya Iran Ayatullah Ali Khamenei. Uzinduzi wa meli hiyo unaiweka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika orodha ya nchi chache zenye teknolojia ya kubuni na kutengeneza meli kubwa za kisasa za kivita.
Katika sherehe za uzinduzi wa meli hiyo ya kivita, Amiri Jeshi wa majeshi ya Iran alikagua sehemu mbalimbali za meli ya Jamaran na kushuhudia kwa karibu sifa makhsusi za mafanikio hayo makubwa ya kitaifa.
Meli ya kivita ya Jamaran ni miongoni mwa meli zinazofanyakazi katika nyanja tatu tofauti za mashambulizi ya anga, juu ya maji na chini ya maji.
Amani, Saada na Uadilifu, Ujumbe Mpya na wa Wazi wa Taifa la Iran kwa Mataifa Yote
Amani, Saada na Uadilifu, Ujumbe Mpya na wa Wazi wa Taifa la Iran kwa Mataifa Yote
Ayatullah Ali Khamenei, Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumanne Oktoba 6, 2009 ameshiriki katika sherehe za kuhitimu mafunzo, kuapishwa na kupewa nishani wanachuo wa Vyuo Vikuu vya kijeshi nchini.
Amesema katika sherehe hizo kwamba maafisa vijana wa jeshi na vijana wakakamavu na waumini katika sekta mbalimbali nchini Iran ni washika ni vongozi wa harakati ya kuelekea kwenye dunia iliyojaa amani, uadilifu na upendo.
Wananchi wa Iran wamewathibitishia walimwengu kwamba njama za maadui haziathiri ari na moyo wa taifa hili
Wananchi wa Iran wamewathibitishia walimwengu kwamba njama za maadui haziathiri ari na moyo wa taifa hili
Taifa lenye imani la Iran leo limetekeleza Sala ya Idul Fitri kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukamilisha funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea sikukuu ya Idi.
Wakazi wa jiji la Tehran wametekeleza sala hiyo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Tehran na mitaa ya kandokando yake wakiongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei

Anwani zilizochaguliwa