Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Matunda ya mazungumzo hayahisiki katika safari za viongozi wa Ulaya nchini Iran
Matunda ya mazungumzo hayahisiki katika safari za viongozi wa Ulaya nchini Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumanne) ameonana na kufanya mazungumzo na Bw. Matteo Renzi, Waziri Mkuu wa Italia hapa mjini Tehran. Amegusia historia ya uhusiano mzuri baina ya nchi mbili za Iran na Italia tangu huko nyuma na namna nchi hizo mbili zinavyokaribisha kuongezwa wigo wa ushirikiano huo na kusema kuwa, tatizo na udhaifu wa safari za mara kwa mara za hivi karibuni za viongozi wa Ulaya nchini Iran ni kule kushindwa kuonekana matunda ya kivitendo na ya waziwazi ya mazungumzo na safari hizo.
Marekani na madola yanayodai kupambana na ugaidi hayasemi ukweli katika uwanja huo
Marekani na madola yanayodai kupambana na ugaidi hayasemi ukweli katika uwanja huo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni (Jumatatu) ameonana na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan ambapo amegusia udharura wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi mbili katika nyuga tofauti za kisiasa, kiuchumi, kimataifa na katika vita dhidi ya ugaidi. Amesema kuwa: Baadhi ya madola hususan Marekani si wakweli katika madai yao ya kupambana na ugaidi, lakini nchi za Kiislamu zinaweza kupambana vilivyo na vitisho vyote vinavyoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa kuwa na ushirikiano wa kweli baina yao.
Uwezo wa jeshi na masuala ya kiroho yameimarishwe zaidi
Uwezo wa jeshi na masuala ya kiroho yameimarishwe zaidi
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) ameonana na makamanda waandamizi wa vikosi vya ulinzi vya Iran na kusema kuwa kielelezo cha "utambulisho wa pamoja" wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa, kwa wakati mmoja vina uwezo wa kufanya opereseheni za kijeshi na wakati huo huo vina misukumo na misimamo ya kimaanawi na kidin.
Ninaunga mkono hatua yoyote yenye maslahi kwa taifa
Ninaunga mkono hatua yoyote yenye maslahi kwa taifa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo adhuhuri (Jumatano) na katika muendelezo wa vikao vya sikukuu ya Nairuzi ameonana na kuhutubia majimui ya viongozi wa serikali, wajumbe wa Kamati Kuu ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) viongozi wa ngazi za juu wa chombo cha Mahakama na viongozi wa taasisi na asasi nyingine nchini. Amewashukuru viongozi hao hususan viongozi wa serikali kwa juhudi na kazi kubwa inayofanywa na serikali katika utekelezaji wa siasa za uchumi ngangari, amelitaja suala la kudumisha upendo na maelewano pamoja na umoja na mshikamano baina ya viongozi nchini kuwa ni jambo muhimu sana katika ufanikishaji wa siasa hizo.
Uchumi ngangari utalinda njia ya kimapinduzi ya Iran
Uchumi ngangari utalinda njia ya kimapinduzi ya Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika siku ya kwanza ya mwaka mpya (wa Kiirani wa 1395 Hijria Shamsia) ametoa hotuba muhimu mbele ya hadhara kubwa ya wafanya ziara na majirani wa Haram toharifu ya Imam Ridha AS. Katika hotuba hiyo muhimu Ayatullah Khamenei amebainisha maana halisi na malengo ya siri na hatari sana ya fikra za watu za kusalimu amri ambazo Marekani naa baadhi ya watu hapa nchini wanataka kuziingiza katika fikra za taifa la Iran kwa kuonesha njia mbili za uongo na za kujibunia. Vilevile ametoa mapendekezo kumi ya kimsingi ya kufanikisha kaulimbiu ya uchukuaji hatua na utekelezaji wa kivitendo katika uwanja wa uchumi ngangari na kusisitiza kuwa: Njia hii ya kimantiki na wakati huo huo ya kimapinduzi itailinda na kuipa kinga Iran azizi mbele ya vitisho na vikwazo.
Sera kuu za Iran ni kushirikiana na nchi za Asia
Sera kuu za Iran ni kushirikiana na nchi za Asia
Katika mazungumzo yake ya alasiri ya leo na Rais Truong Tan Sang wa Vietnam, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiufundi, kibiashara na kiutamaduni kwa ajili ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili na kusema kuwa: "Ushujaa na mapambano ya taifa la Vietnam na shakhsia wake wakubwa kama Ho Chi Minh na Jenerali Giap ambao walikabiliana na kupambana na wavamizi wa kigeni ni jambo ambalo limelifanya taifa la Vietnam liheshimike na liwe na hadhi mbele ya taifa la Iran, na mfungamano huu unapaswa kuandaa mazingira mwafaka ya kuimarisha zaidi uhusiano".
Chuo kikuu cha kidini cha Qum kinapaswa kuendelea kuwa cha kimapinduzi
Chuo kikuu cha kidini cha Qum kinapaswa kuendelea kuwa cha kimapinduzi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumanne) ameonana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) ya Qum na sambamba na kubainisha hadhi na nafasi muhimu isiyo na mbadala na yenye taathira kubwa ya Hawza za kidini katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini ameashiria baadhi ya njama zinazofanywa kwa ajili ya kuondoa mapinduzi katika Hawza na chuo kikuu cha kidini. Amesisitiza kuwa: Hawza ya Qum inapaswa iendelee kuwa chuo cha kimapinduzi na kitovu cha Mapinduzi na kwamba ili kuweza kulifikia lengo hilo kunahitajika fikra, tadbiri na mipangilio mizuri.
Wananchi wametimiza wajibu wao ipasavyo katika uchaguzi, sasa ni zamu ya viongozi
Wananchi wametimiza wajibu wao ipasavyo katika uchaguzi, sasa ni zamu ya viongozi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Alkhamisi) alikuwa na kikao cha mwisho na mkuu na wajumbe wa Baraza la Nne la Wanavyuoni Wataalamu linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Mku wa Iran. Katika mkutano huo Ayatullah Khameni ametoa hotuba muhimu sana akiwashukuru wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi na kwa sura yenye maana maalumu katika uchaguzi wa Februari 26 na kutangaza utiifu na mapenzi yao kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, na amebainisha sifa kadhaa maalumu za uchaguzi huo na majukumu muhimu zaidi pamoja na vipaumbele vya Baraza la Wanavyuoni Wataalamu na wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika duru hii mpya.
Wafanyabiashara wa Uswisi wawekeze Iran na kuboresha biashara ya pande mbili
Wafanyabiashara wa Uswisi wawekeze Iran na kuboresha biashara ya pande mbili
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amefanya mazungumzo na Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi aliyeko safarini hapa nchini akiashiria historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili na taswira nzuri ya mwenendo wa Uswisi katika fikra za Wairani na amekaribisha suala la kuzidishwa ushirikiano wa kiuchumi na kielimu wa pande mbili. Amesema kiwango cha mabadilishano ya kibiashara kati ya Iran na Uswisi ni kidogo na hakina mlingano, na kusisitiza kwamba, wafanyabiashara na wawekezaji wa Uswisi wanaweza kuboresha mizani hiyo kwa kuelewa vyema uwezo mkubwa wa Iran.
Madai ya kuwepo bunge na serikali na bunge dhidi ya serikali ni urongo mtupu
Madai ya kuwepo bunge na serikali na bunge dhidi ya serikali ni urongo mtupu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatano) ametoa hotuba muhimu katika hadhara kubwa ya wananchi wa Najafabad akitoa maelezo ya kina kuhusu msamiati wa "misimamo ya kati na misimamo mikali" na kuwataka wananchi wote hususan viongozi na wanasiasa kuwa macho mbele ya njama za adui za kutaka kuzusha kambi mbili bandia na za kutwisha katika nga ya sasa ya uchaguzi. Amesema kuwa uchaguzi ni medani ya kutunisha kifua kitaifa, kuonesha uaminifu, kusimama kidete kwa taifa na kulinda heshima na kujitawala. Amesisitiza kuwa, watu wote wanaoitakia izza na heshima Iran ya Kiislamu wanapaswa kushiriki katika uchaguzi wa Ijumaa ijayo.
Kueneza maarifa ya Kiislamu kutaimarisha msaada wa wananchi kwa serikali ya Azerbaijan
Kueneza maarifa ya Kiislamu kutaimarisha msaada wa wananchi kwa serikali ya Azerbaijan
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amefanya mazungumzo na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan ofisi kwake hapa mjini Tehran. Ayatullah Khamenei ameashiria uhusiano mzuri wa kisiasa na masuala mengi yanayozikutanisha pamoja Iran na Azerbaijan hususan masuala ya kidini na kimadhehebu ya mataifa hayo mawili na kusema: Kueneza maarifa ya Kiislamu na kuheshimu madhihirisho na nembo za kidini ni sababu ya msaada wa wananchi dhidi ya vitisho vya adui.
Watu kwenye uchaguzi, wafanye kinyume na matakwa ya adui
Watu kwenye uchaguzi, wafanye kinyume na matakwa ya adui
Leo Asubuhi Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameonana na umati mkubwa wa maelfu ya watu wa matabaka mbalimbali kutoka Azarbaijan Mashariki, na huku akitoa shukrani zake za dhati kwa taifa la Iran kutokana na ushiriki wao mkubwa katika maandamano ya tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, amesema kuwa ushiriki huo mkubwa unathibitisha wazi azma thabiti, msimamo imara na mwamko wa wananchi. Amesisitiza kwamba uchaguzi ujao wa tarehe 26 Februari nchini pia utakuwa ni dhihirisho la mwamko wa taifa na uteteaji wake wa mfumo wa Kiislamu, kujitawala na heshima ya taifa.
Taifa la Syria ndilo linalopaswa kuchukua uamuzi kuhusu mustakbali wa Syria si Marekani
Taifa la Syria ndilo linalopaswa kuchukua uamuzi kuhusu mustakbali wa Syria si Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amemkaribisha ofisi kwake na kufanya mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Khamenei ameashiria mtazamo chanya na wa upendeleo wa Iran katika suala la kuzidisha ushirikiano na nchi za Kiafrika tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kusema: Madola makubwa ya kibeberu yanapinga kuwapo uhusiano mzuri kati ya Iran na nchi za Afrika na ndiyo sababu ya vita, mapigano na wafadhili wa makundi ya kigaidi; hata hivyo tiba ya matatizo yote hayo imo katika kukurubiana zaidi nchi zinazojitawala na kuzidisha ushirikiano wao.
Maandamano makubwa ya wananchi tarehe 22 Bahman yatawavunja moyo maadui
Maandamano makubwa ya wananchi tarehe 22 Bahman yatawavunja moyo maadui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi ameonana na makamanda na majimui ya maafisa wa Jeshi la Anga na wa kikosi maalumu cha ulinzi wa anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kuyataja maadhimisho ya Bahman 22 (ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu) na uchaguzi kuwa ni sikukuu mbili zenye maana pana kwa taifa la Iran. Vilevile amesisitiza wajibu wa kujitokeza kwa wingi wananchi na kwa njia ya kutoa pigo kwa adui katika maandamano ya kuadhimisha Bahman 22 (Februari 11) mwaka huu.
Ulaya inapaswa kurekebisha udhaifu wake wa kutokuwa huru mbele ya Marekani
Ulaya inapaswa kurekebisha udhaifu wake wa kutokuwa huru mbele ya Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei jioni ya leo (Jumatatu) amemkaribisha ofisini kwake Bw. Alexis Tsipras, Waziri Mkuu wa Ugiriki. Katika mazungumzo yake na mgeni huyo Ayatullah Khamenei ameshiria historia inayong'ara ya uhusiano wa kiutamaduni na kiustaarabu baina ya Iran na Ugiriki na kusisitiza kuwa, ziara ya Waziri Mkuu huyo wa Ugiriki nchini Iran inaweza kuwa mwanzo mzuri wa kuzidisha kiwango cha mabadilishano ya kibiashara na kuweka mikakati ya ushirikiano wa muda mrefu baina ya nchi mbili.
Hotuba za Imam ndiyo msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Hotuba za Imam ndiyo msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi ameonana na Admeli Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa pamoja na manaibu na wataalamu wa sekretarieti ya baraza hilo. Ameashiria namna istilahi na neno "usalama" lilivyo tata na lilivyo na vipengee vingi tofauti katika dunia ya leo na kulitaja jukumu la Baraza Kuu la Usalama wa Taifa kuwa ni kuchukua maamuzi kwa kuangalia upana na vipengee vyote vya neno usalama.
Uhusiano wa kistratijia wa Iran na China ni sahihi na wenye hikima
Uhusiano wa kistratijia wa Iran na China ni sahihi na wenye hikima
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo jioni (Jumamosi) amezungumza na Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya Watu wa China na ujumbe alioandamana nao ambapo amegusia historia kongwe ya uhusiano wa kibiashara na kiutamaduni baina ya mataifa mawili ya Iran na China na kusisitiza kuwa: Serikali na taifa la Iran muda wote lilikuwa na linaendelea kufuatilia suala la kustawisha uhusiano wake na nchi huru na zinazoaminika kama vile China na ni kwa sababu hiyo ndio maana makubaliano baina ya marais wa Iran na China ya kuwa na uhusiano wa kiistratijia wa miaka 25 yakawa ni makubaliano sahihi kabisa na ya hekima sana.
Kiongozi Muadhamu: Sheria zinapaswa kuheshimiwa ipasavyo
Kiongozi Muadhamu: Sheria zinapaswa kuheshimiwa ipasavyo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) amehutubia hadhara kubwa ya maafisa wanaosimamia na kuendesha uchaguzi wa awamu ya kumi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na uchaguzi wa awamu ya tano wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu). Ametoa ufafanuzi kuhusiana na adabu na mambo yanayoweza kudhamini ushindani salama katika uchaguzi amesema kuwa, taifa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo washindi watakaopata fakhari kubwa kwa kuweko ushindani wenye nguvu wa kitaifa katika medani ya uchaguzi. Vilevile amewabainishia viongozi nchini nukta kadhaa muhimu kuhusiana na kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 (JCPOA) na kuwaasa viongozi nchini akiwaambia: Marekani ni ile ile Marekani ya zamani, tahadharini na hadaa zake hata katika utekelezaji wa haya matokeo ya hivi sasa ya mazungumzo ya nyuklia.
Dawa ya matatizo ya Afghanistan ni umoja na mshikamano wa kaumu zote
Dawa ya matatizo ya Afghanistan ni umoja na mshikamano wa kaumu zote
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei,leo asubuhi (Jumanne) ameonana na Bw. Abdullah Abdullah Afisa Mtendaji Mkuu wa serikali ya Afghanistan na kulitaja suala la umoja baina ya makabila na kaumu zote za Afghanistan kuwa ndio utatuzi wa matatizo ya nchi hiyo na huku akiashiria historia na mambo mengi yanayosahilisha kuweko ushirikiano baina ya Iran na Afghanistan amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inauhesabu usalama, utulivu na maendeleo ya Afghanistan kuwa ni usalama na maendeleo yake.
Wamarekani wanakodolea jacho la tamaa uchaguzi wa Iran
Wamarekani wanakodolea jacho la tamaa uchaguzi wa Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na maimamu wa Swala za Ijumaa kutoka pembe zote za Iran na huku akiashiria utukufu na nafasi ya juu mno ya Swala ya Ijumaa amesema kuwa, sala hiyo ni kitovu cha imani, busuri na maadili mema na kwamba jukumu kuu la maimamu wa Swala za Ijumaa ni kubainisha uhakika wa mambo na kuwa viongozi wa kiutamaduni na kisiasa katika jamii. Vilevile amesema kuwa, uchaguzi ni jambo muhimu mno na kwa hakika ni neema kubwa sana.

Anwani zilizochaguliwa