Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Mkono wa adhabu ya Mwenyezi Mungu utawakumba wanasiasa wa Aal Saud
Mkono wa adhabu ya Mwenyezi Mungu utawakumba wanasiasa wa Aal Saud
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo (Jumapili) katika darsa yake ya masomo ya juu ya fiqhi amelaani vikali jinai kubwa iliyofanywa na Saudi Arabia ya kumuua shahidi mwanazuoni muumini na madhlumu, Sheikh Nimr Baqir al Nimr na kusisitiza kwamba, dunia inapaswa kubeba majukumu yake mbele ya jinai hiyo na jinai nyingine mfano wake zinazofanywa na Saudi Arabia huko Yemen na Bahrain. Amesema hapana shaka kuwa, athari ya damu iliyomwagwa kidhulma ya shahidi huyu madhulumu itaenea kwa kasi na ulipizaji kisasi wa Mwenyezi Mungu utawakumba wanasiasa wa utawala wa Aal Saud.
Umma wa Kiislamu unapaswa kujenga ustaarabu mpya wa Kiislamu
Umma wa Kiislamu unapaswa kujenga ustaarabu mpya wa Kiislamu
Sambamba na kuwadia mwezi 17 Mfunguo Sita, siku ya kuadhimisha Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Imam Jafar Sadiq AS, viongozi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wageni walioshiriki kwenye mkutano wa Umoja wa wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu na majimui ya wananchi wa matabaka tofauti, leo asubuhi wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei mjini Tehran.
Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kutoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Bwana Mtume mtukufu SAW na Imam Sadiq AS ameashiria suala la kupulizwa roho ya uhai na umaanawi wa kweli baada ya ujio wa Mtume wa Uislamu na namna neema ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW na kudhihiri Uislamu ilivyoweza kuhuisha dunia iliyokuwa imekufa na kuteketezwa na ujahilia.
Uongozi na nguvu kazi nzuri vinafanya muujiza
Uongozi na nguvu kazi nzuri vinafanya muujiza
Ayatullah Khamenei ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran adhuhuri ya leo (Jumapili) amehutubia hadhara ya makamanda na maafisa wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu. Ameashiria umuhimu wa bahari na maendeleo makubwa ya Jeshi la Majini katika kutumia fursa za baharini na kusisitiza udharura wa kudumishwa maendeleo na ujenzi wa Jeshi hilo. Amesema: Nguvu kazi njema, yenye utanashati, fikra na uongozi sahihi sambamba na kusimama kidete, azma kubwa, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na matumaini ya mustakbali mwema ndiyo mambo yanayoweza kuisaidia zaidi Iran ya Kiislamu kufikia nafasi kubwa, ya kihistoria na inayonasibiana na hadhi yake.
Tutatetea harakati ya Wapalestina kwa nguvu zetu zote
Tutatetea harakati ya Wapalestina kwa nguvu zetu zote
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asubuhi ya leo (Jumatano) amehutubia hadhara kubwa ya makamanda 2500 wa vikosi vya wapiganaji wa kujitolea wa Basiji waliokwenda kuonana naye akiitaja taasisi hiyo kuwa ni mwakilishi mwenye baraka nyingi na anayestawi wa taifa. Amebainisha mbinu za kiadui zinazotumiwa na ubeberu dhidi ya taifa la Iran na kusisitiza kuwa: Katika mpambano na vita halisi vya kambi ya ubeberu na kambi ya kupigania utambulisho na uhuru, taifa la Iran litatekeleza wajibu wake wa kuwatetea watu wanaodhulumiwa hususan taifa shujaa la Palestina katika Intifadha ya Ukingo wa Magharibi.
Kuna udhaura wa kukabiliana na siasa za Marekani za kutaka kubadili utambulisho wa mataifa
Kuna udhaura wa kukabiliana na siasa za Marekani za kutaka kubadili utambulisho wa mataifa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya leo ameonana na kufanya mazungumzo na Rais Evo Morales wa Bolivia aliyeko safarini hapa nchini. Ayatullah Ali Khamenei amepongeza kusimama imara na kishujaa kwa Bolivia na baadhi ya nchi nyingine za Amerika ya Latini dhidi ya sera za kutumia mabavu na dhulma za kambi ya ubeberu na akasema: Siasa hatari za Marekani duniani na katika eneo la Amerika ya Kusini zinalenga kubadili utambulisho wa vijana. Amesisitiza kuwa, kuna udharura wa kukabiliana na siasa hizo za kibeberu kwa kuimarisha azma na kuzidisha uhusiano na ushirikiano.
Nchi za Kiislamu zinapaswa kutafuta njia ya kivitendo ya kukabiliana na magaidi
Nchi za Kiislamu zinapaswa kutafuta njia ya kivitendo ya kukabiliana na magaidi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kabla ya adhuhuri ya leo amemkaribisha ofisini kwake Waziri Mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal na ujumbe unaoandamana naye.
Katika mazungumzo hayo Ayatullah Ali Khamenei ameashiria misimamo ya kisiasa inayokaribiana ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Algeria na akasema: Mbali na kukaribiana misimamo hiyo ya kisiasa, taifa la Iran lina mtazamo chanya kuhusu nchi na wananchi wa Algeria na suala hilo linatokana na jihadi ya Waalgeria dhidi ya ukoloni katika kipindi cha Mapinduzi ya Algeria.
Wamarekani hawapaswi kuruhusiwa kuzungumzia suala la kuigawa Iraq
Wamarekani hawapaswi kuruhusiwa kuzungumzia suala la kuigawa Iraq
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi (Jumanne) ameonana na kuzungumza ofisini kwake na Rais Fuad Masum wa Iraq pamoja na ujumbe alioandamana nao.
Katika Mazungumzo hayo Kiongozi Muadhamu amesema kuwa uhusiano mkubwa iliopo kati ya nchi na mataifa mawili ya Iran na Iraq ni wa kina, kihistoria na ulio juu ya uhusiano wa kawaida wa nchi jirani na zilizo katika eneo moja.
Akisisitiza udharura wa kulindwa umoja wa taifa la Iraq, Ayatullah Khamenei amesema: Taifa la Iraq ni taifa kubwa na lililo na historia kongwe na lenye vijana shupavu na wenye mwamko.
Lengo la Marekani ni kutokomeza mapambano ya taifa la Venezuela
Lengo la Marekani ni kutokomeza mapambano ya taifa la Venezuela
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mpainduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na kuzungumza na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ambapo amesifu mapambano na harakati ya kuvutia ya Venezuela katika kukabiliana na siasa za uistikbari na kusisitiza: Leo siasa siasa za uistikbari ni kama balaa kubwa lililoikumba jamii ya mwanadamu na njia pekee ya maendeleo na ushindi kwa nchi huru zinazojitawala ni kupambana na kuwategemea wananchi katika vita vya matakwa.
Miungano ya kimataifa eti ya kupambana na ugaidi haiwezi kuaminiwa
Miungano ya kimataifa eti ya kupambana na ugaidi haiwezi kuaminiwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei kabla ya adhuhuri ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria aliyeko safarini hapa nchini. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Khamenei amesema kuwa, kuna udharura wa kuzidishwa ushirikiano baina ya nchi za Kiislamu katika kulinda utambulisho wa Uislamu na Waislamu. Amesisitiza kuwa, miungano ya kimataifa inayodai kupambana na mirengo ya kigaidi haiwezi kuaminiwa kwa njia yoyote ile kwa sababu waharibifu hao hususan Marekani ndio waanzilishi au waungaji mkono wa nyuma ya pazia wa makundi ya kigaidi kama lile la Daesh.
Marekani ina mpango wa muda mrefu wa kulidhibiti eneo la magharibi mwa Asia
Marekani ina mpango wa muda mrefu wa kulidhibiti eneo la magharibi mwa Asia
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya leo (Jumatatu) amemkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia ofisini kwake hapa mjini Tehran. Ayatullahil Ali Khamenei amekaribisha suala la kuimarishwa zaidi ushirikiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa na kuipongeza Moscow kwa mchango wake wenye taathira katika masuala ya kieneo hususan katika kadhia ya Syria. Amesema kuwa njama za muda mrefu za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati zina madhara kwa mataifa na nchi zote hususan Iran na Russia na kwamba njama hizo zinapaswa kuzimwa kwa kuwa macho na kushirikiana kwa karibu.
Uislamu ni dini ya udugu, upendo na kheri
Uislamu ni dini ya udugu, upendo na kheri
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya leo (Jumapili) amezungumza na Rais Gurbanguly Berdimuhamedow wa Turkmenistan aliyemtembelea ofisi kwake hapa mjini Tehran. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria uhusiano wa kirafiki wa Iran na Turkmenistan na nyanja nyingi zilizopo kwa ajili ya kustawisha zaidi ushirikiano wa pande mbili na kukabiliana na sera za kuzusha vita na mapigano katika eneo hili na kusema: Njia ya kukabiliana na mirengo ya kigaidi na kuzima ushawishi wao ni kuwashirikisha wananchi katika shughuli sahihi za Kiislamu na kuimarisha harakati za kifikra za Kiislamu zenye misimamo ya wastani na ya kimantiki.
Vijana wenye imani na wanamapinduzi katika vyuo vikuu wapewe uwanja
Vijana wenye imani na wanamapinduzi katika vyuo vikuu wapewe uwanja
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amehutubia hadhara ya wakuu wa vyuo vikuu, vituo, taasisi za elimu ya juu na bustani za sayansi na teknolojia na vituo vya utafiti hapa nchini. Ameeleza kwa urefu historia, turathi na tajiriba ya kielimu hapa nchini hususan katika kipindi cha kabla na baada ya kudhihiri Uislamu na nafasi na mchango wa vyuo vikuu katika historia ya sasa hususan katika harakati ya Kiislamu na baada ya Mapinduzi ya Kiislamu. Vilevile amesisitiza udharura wa vyuo vikuu na vituo vya kielimu kuweka mipango kwa ajili ya kutumia turathi na tajiriba kubwa ya kielimu kwa shabaha ya kujenga ustaarabu wa kisasa wa Kiislamu.
Mapambano dhidi ya ubeberu yanaungwa mkono na akili na tajiriba
Mapambano dhidi ya ubeberu yanaungwa mkono na akili na tajiriba
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumanne) amehutubia hadhara ya maelfu ya wanachuo na wanafunzi wa wengine hapa nchini akisema kuwa mapambano ya taifa la Iran dhidi ya ubeberu ni mapambano ya kimantiki, kiakili na yanayotegemea tajiriba na uzoefu wa kihistoria. Ameashiria matatizo na madhara yaliyotokana na kuiamini Marekani na upeo mfupi wa kifikra wa baadhi ya wanasiasa katika historia ya sasa ya nchi hii na kusema: Marekani ndiyo ileile Marekani ya zamani lakini baadhi ya watu waovu au wapumbavu wanafanya jitihada za kulisahaulisha na kulighafilisha taifa na adui huyo anayefanya njama ili Marekani iweze kupiga hanjari mgongoni katika kipindi mwafaka.
Suala la nchi nyingine kuchukua maamuzi juu ya nfumo wa serikali ya Syria ni uzushi hatari sana
Suala la nchi nyingine kuchukua maamuzi juu ya nfumo wa serikali ya Syria ni uzushi hatari sana
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi (Jumapili) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje, mabalozi pamoja na manaibu balozi wa Jamhuri ya Kiislamu (na kubainisha misingi na stratijia thabiti na imara za siasa za nje katika katiba na mambo ya lazima yanayofungamana na misingi na siasa hizo) na kubainishia njia za kimantiki na madhubuti za Iran katika utatuzi wa masuala muhimu ya kieneo, yakiwemo ya Syria, Yemen na Bahrain. Amesisitiza kuwa malengo ya Marekani na ya Iran yanatofautiana kwa digrii 180.
Maafa ya kusikitisha ya Mina hayapasi kusahauliwa
Maafa ya kusikitisha ya Mina hayapasi kusahauliwa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo (Jumatatu) ameonana na maafisa wa kusimamia ibada ya Hija wa Iran na kuyataja maafa machungu mno na ya kusikitisha sana ya Mina kuwa ni miongoni mwa mitihani ya Mwenyezi Mungu. Amezilaumu tawala za nchi mbalimbali na hususan tawala za nchi za Magharibi na mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu kwa kunyamazia kimya msiba huo mkubwa kusisitiza kuwa: Tukio hilo halipaswi kabisa kusahauliwa na kwamba chombo cha diplomasia na Taasisi ya Hija ya Iran vina wajibu wa kulifuatilia ipasavyo suala hilo.
Kubakia hai malengo na nara za Mapinduzi kunamkasirisha adui
Kubakia hai malengo na nara za Mapinduzi kunamkasirisha adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumatano) amehutubia hadhara ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana wenye vipaji bora vya kielimu nchini akitoa nasaha na tahadhari muhimu kwa watu wenye vipawa na viongozi nchini. Pia amesisitizia ulazima wa kuipa uzito wa hali ya juu taasisi ya watu wenye vipawa ikiwa ni taasisi ya kitaifa na ya kiistratijia na vilevile kuandaa uwanja wa kuchanua na kutoa msaada wa kielimu vijana hao wenye vipaji katika jamii. Amesema, mashirika ya elimu za kimsingi ni miongoni mwa nguzo kuu za uchumi ngangari na wa kusimama kidete.
Lengo kuu la vita laini vya adui ni kubadili hakika ya Jamhuri ya Kiislamu na itikadi za wananchi
Lengo kuu la vita laini vya adui ni kubadili hakika ya Jamhuri ya Kiislamu na itikadi za wananchi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatatu) amehutubia hadhara ya viongozi na wakurugenzi wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na wajumbe wa baraza linalosimamia utendji wa shirika hilo akieleza malengo ya vita laini iliyoratibiwa, kubwa na ya pande zote ya mfumo wa ubeberu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Amesema kubadilisha itikadi za wananchi ndiyo lengo muhimu zaidi la vita hivyo tata. Ametilia mkazo nafasi ya kipekee ya IRIB katika mpambano huo mkubwa, na kusisitiza udharura wa kuwepo mipango mizuri na ya kitaalamu kwa ajili ya kutimiza majukumu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.
Ni marufuku kuzungumza na Marekani kwa sababu ya madhara yake mengi
Ni marufuku kuzungumza na Marekani kwa sababu ya madhara yake mengi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumatano) amehutubia hadhara ya makamanda na wafanyakazi wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah), familia zao na familia za mashahidi wa jeshi hilo. Ameashiria nafasi na mchango wa vijana wanamapinduzi wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Sepah na vijana shupavu wa kusini katika kulinda usalama wa baharini na kumtia woga adui na akasema: Maadui wanataka kubadilisha mahesabu ya maafisa wa Iran na kubadili fikra za wananchi hususan vijana hivyo wananchi wote wanapaswa kuwa macho na makini.
Imarisheji jeshi kiasi kwamba adui asifikirie kuishambulia Iran
Imarisheji jeshi kiasi kwamba adui asifikirie kuishambulia Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Akhamisi) amehutubia hadhara ya makamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kusema, sababu ya uadui unaofanywa dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kusimama kidete kwa taifa la Iran, uwazi na kutosalimu amri kwake mbele ya siasa za ubeberu. Amesisitiza kuwa vikosi vya jeshi la Iran vinapaswa kuzidisha kasi ya maendeleo na kuzidisha utayarifu wake kwa kadiri kwamba, adui asithubutu hata kuwa na fikra ya kuihujumu Iran.

Anwani zilizochaguliwa