Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Taifa la Iran litajibu uchokozi wa aina yoyote wa adui
Taifa la Iran litajibu uchokozi wa aina yoyote wa adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo (Jumatano) amekutana na maafisa wa Wizaya ya Elimu na walimu kutoka maneo mbalimbali hapa nchini ambapo ameeleza nafasi ya kipekee ya elimu na malezi na vilevile mchango mkubwa na muhimu wa walimu katika malezi ya kizazi chenye imani, maarifa, uoni wa mbali na chenye kujiamini, nishati na matumaini na akasema: Kufikiwa malengo hayo kunategemea utekelezwaji kamili wa hati ya marekebisho makubwa na ya kimsingi katika sekta ya elimu.
Ufunguo wa kutatua matatizo ya kiuchumi uko ndani ya nchi
Ufunguo wa kutatua matatizo ya kiuchumi uko ndani ya nchi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya leo (Jumatano) amekutana na maelfu ya wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ambapo ameeleza nyadhifa za maafisa wa serikali, asasi na vyombo mbalimbali vinavyojihusisha na masuala ya uzalishaji wa ndani ya nchi. Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza udharura wa kupambana ipasavyo na ubadhirifu na magendo na akasema: Ufunguo wa matatizo ya kiuchumi ya wananchi na matatizo ya jamii ya wafanyakazi uko katika kuimarishwa na kustawishwa uzalishaji wa ndani ya nchi.
Nguvu inayotakikana katika Uislamu inapaswa kuambatana na uadilifu na urehemevu
Nguvu inayotakikana katika Uislamu inapaswa kuambatana na uadilifu na urehemevu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo (Jumapili) amehutubia hadhara ya washiriki katika kongamano la makamanda, wakurugenzi na viongozi wa vitendo vya itikadi na siasa wa Jeshi la Polisi na kusema kuwa, jeshi hilo ni dhihirisho la kujitawala na usalama wa Jamhuri ya Kiislamu. Amesisitiza kuwa jukumu kubwa zaidi la Jeshi la Polisi ni kuleta amani ya mtu binafsi, ya jamii, ya kimaadili na ya kinafsi katika jamii. Ameongeza kuwa sharti la kuweza kuleta amani ni kuwa na nguvu Jeshi la Polsi lakini nguvu hiyo inapaswa kuandamana na uadilifu, murua na urehemevu.
Iran inapaswa kuzidisha uwezo wake wa kujihami siku baada ya siku
Iran inapaswa kuzidisha uwezo wake wa kujihami siku baada ya siku
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo ametubua hadhara ya makamanda, wafanyakazi na familia za mashahidi wa jeshi la Iran akiliamuru kulinda, na kuimarisha muono wake wa mbali na mwelekeo wa kidini na kimapinduzi, kuzidisha uwezo wa kujihami na wa kisilaha na kuwa tayari kiroho. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi na haitakuwa tishio kwa eneo hili na nchi jirani lakini itajibu uchokozi wa aina yoyote kwa nguvu zake zote.
Iran inatambua usalama na maendeleo ya Afghanistan kuwa ni usalama na maendeleo yake
Iran inatambua usalama na maendeleo ya Afghanistan kuwa ni usalama na maendeleo yake
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khameni alasiri ya leo amemkaribisha Rais wa Afghanistan ofisini kwake. Ayatullah Khamenei ameashiria uhusiano na mambo mengi ya kiutamaduni na kihistoria yanayozikutanisha pamoja nchi hizo mbili na kusema, mchango wa maulama na wana fasihi wa Afghanistan katika kustawisha na kueneza maarifa ya Kiislamu na lugha ya Kifarsi ni mkubwa na muhimu.
Jinai za Saudia nchini Yemen zinashabihiana na jinai za Wazayuni huko Gaza
Jinai za Saudia nchini Yemen zinashabihiana na jinai za Wazayuni huko Gaza
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia mjumuiko mkubwa wa wanawake, washairi na wasomaji wa tungo za Ahlulbaiti wa Mtume (saw) na sambamba na kuwapongeza Waislamu kwa mnasaba wa kuadhimisha siku aliyozaliwa Bibi Fatimatu Zahra (as), amezungumzia masuala muhimu sana kuhusu mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi ya 5+1 na vilevile matukio ya Yemen. Amesema jinai zinazofanywa na Saudi Arabia huko Yemen zinashabihiana na zile zinazofanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza huko Palestina na kutaka jinai hizo zikomeshwa mara moja.
Njia ya kuhitimishwa mgogoro wa Yemen ni kusitishwa mashambulizi
Njia ya kuhitimishwa mgogoro wa Yemen ni kusitishwa mashambulizi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei amesema leo katika mazungumzo yake na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki aliyeko safarini hapa nchini kwamba mwamko wa Kiislamu ndiyo sababu kuu ya wasiwasi wa maadui wa Uislamu. Ayatullah Khamenei ameashiria njama na mipango ya maadui kwa ajili ya kukabiliana na mwamko wa Kiislamu na akasema: Hii leo Marekani na Wazayuni wanafurahishwa na hitilafu za ndani katika baadhi ya nchi za Waislamu na njia ya utatuzi wa matatizo hayo ni ushirikiano wa nchi za Kiislamu na kuchukuliwa hatua za kivitendo na zinazofaa.
Vikwazo viondolewe baada tu ya kufikiwa makubaliano
Vikwazo viondolewe baada tu ya kufikiwa makubaliano
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo (Jumamosi) katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 1934 Hijria Shamsia amehutubia hadhara kubwa ya makumi ya maelfu ya wananchi waliokwenda kuzuru Haram ya Imam Ali bin Mussa Ridha (as) katika uwanja wa Imam Khomeini. Katika hotuba hiyo muhimu, Ayatullah Khamenei ametoa maelezo kuhusu kaulimbiu ya mwaka mpya ya “Serikali na Wananchi, Mshikamano na Maelewano” na kusisitiza juu ya wadhifa wa pande mbili wa uungaji mkono wa wananchi kwa serikali halali na ya kisheria na ulazima wa viongozi wa serikali kuwa na kifua kipana na kustahamili ukosoaji wa kimantiki.
Tukabiliane na hujuma dhidi ya Uislamu kwa kuarifisha Uislamu halisi
Tukabiliane na hujuma dhidi ya Uislamu kwa kuarifisha Uislamu halisi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Alkhamisi amekutana na Mwenyekiti na wawakilishi wa Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran ambapo amesema kutekelezwa Uislamu kamili ndiyo takwa la Mwenyezi Mungu na lengo kuu la utawala wa Jamhuri ya Kiislamu hapa nchini. Ameashiria udharura wa kuoneshwa Uislamu halisi mbele ya njama za mabeberu za kutaka kueneza hofu kuhusu Uislamu katika mataifa mbalimbali na akasema: Kuna udharura wa kujiepusha na mtazamo wa kijuujuu wakati wa kuchunguza sababu na njia za kukabiliana na changamoto zilizopo na kuchunguza kwa kina sababu za mambo mbalimbali ili kuweza kuyaendesha vyema na kwa njia za kimantiki.
Utatuzi wa kuchafuliwa mazingira unahitaji kazi na bidii na si kampeni na propaganda
Utatuzi wa kuchafuliwa mazingira unahitaji kazi na bidii na si kampeni na propaganda
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amekutana na wafanyakazi wa Idara ya Hifadhi ya Mazingira ambapo amesema kuwa utatuzi wa matatizo ya mazingira kama uchafuzi wa hewa, vimbunga vya vumbi na uvamizi wa misitu, nyika na malisho na maeneo ya umma unahitaji mipango, tadbiri na ufuatiliaji wa kweli na wa mara kwa mara wa vyombo husika.
Kaulimbiu ya
Kaulimbiu ya "Sisi Tunaweza" ionyeshwe kivitendo kwa wananchi
Hotuba iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei katika kikao cha wanachama wa kamati ya maandalizi ya Siku ya Taifa ya Wahandisi hapo tarehe 6/11/93 Hijria Shamsia (26 Januari 2015) ilisambazwa leo asubuhi katika kongamano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran. Katika hotuba hiyo Kiongozi Muadhamu alisisitiza kuwa kaulimbiu ya "Sisi Tunaweza" inapaswa kuonyeshwa kivitendo kwa wananchi.
Adui anapinga asili ya Mapinduzi ya Kiislamu
Adui anapinga asili ya Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amekutana na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Azarbaijan Mshariki ambapo amelipongeza taifa la Iran kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman (11 Februari, siku ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini). Katika hotuba yake muhimu kwenye hadhara hiyo, Ayatullah Khamenei ameeleza hali ya kiuchumi ya Iran na njia za utatuzi wa mambo mbalimbali hususan udharura wa kutekelezwa sera za uchumi wa kimapambano. Ameashiria pia mivutano iliyopo, masharti ya Marekani na vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran na akasema: Taifa la Iran daima limeonesha kuwa lina idara imara, na katika suala la vikwazo taifa hili linaweza kuzima njama hizo.
Makubaliano ya Iran na 5+1 yawe ya awamu moja na yajumuishe vitu vyote
Makubaliano ya Iran na 5+1 yawe ya awamu moja na yajumuishe vitu vyote
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumapili) ameonana na makamanda na wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu na akibainisha sababu na lengo kuu la uadui wa miaka 36 na unaondelea hadi hivi sasa wa Wamarekani na kosa lao la kimahesabu kwa ajili ya kutaka kulipigisha magoti na kulidhalilisha taifa la Iran. Amegusia miamala na hatua za kimantiki na zenye ushahidi madhubuti za Iran katika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kuwa: Siku ya Bahman 22 Taifa la Iran litaonesha kwamba haliwezi kukubaliana na ubeberu na litatoa kipigo kwa mdhalilishaji yeyote yule.
Maendeleo katika sekta ya nano yawe kigezo cha maendeleo katika sekta nyingine
Maendeleo katika sekta ya nano yawe kigezo cha maendeleo katika sekta nyingine
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumamosi) ametembelea maonyesho ya mafanikio ya teknolojia ya nano ya Iran katika Husainia ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) mjini Tehran kwa muda wa saa moja na nusu na kuona kwa karibu mchakato wa jitihada na maendeleo makubwa ya kielimu ya wanasayansi na wasomi vijana wa Iran katika teknolojia ya nano.
Iran itaendelea kusimama imara hadi Palestina itakapokombolewa
Iran itaendelea kusimama imara hadi Palestina itakapokombolewa
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kadhia ya Palestina ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete hadi pale malengo ya Palestina yatakapotimia na hapana shaka kuwa vijana watashuhudia siku hiyo.
Kuonesha masuala ya kimaanawi katika michezo kunadhihirisha istiqama ya taifa la Iran
Kuonesha masuala ya kimaanawi katika michezo kunadhihirisha istiqama ya taifa la Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na mabingwa na wanamichezo wengine walioshiriki katika mashindano ya Asia na Para Asia huko Incheon, Korea Kusini na huku akiashiria nafasi ya ushindi unaopatikana kwenye medani mbalimbali za michezo katika kuleta hisia za kujivunia kitaifa wananchi, amekutaja kusimama kidete kimaanawi kunakofanywa na wanamichezo na mabingwa katika kuhifadhi na kueneza matukufu na nara za kidini mbele ya mamilioni ya watu kuwa ni jambo muhimu mno.
Kushuka kwa bei ya mafuta ni harakati ya kisiasa isiyo ya kiuchumi
Kushuka kwa bei ya mafuta ni harakati ya kisiasa isiyo ya kiuchumi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo jioni (Jumamosi) ameonana na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na sambamba na kuisifu misimamo na hatua zilizochukuliwa na Venezuela katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel, ameitaja sababu inayoifanya kambi ya kiistikbari na kibeberu iifanyie uadui na kuishinikiza Venezuela kuwa ni msimamo wake huo wa kishujaa, wenye taathira na wa kiistratijia katika eneo la Amerika ya Latini na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya kweli na isiyotetereka ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano wake wa pande zote na Venezuela.
Moyo wa mapambano na kusimama kidete ni kielelezo cha heshima ya jeshi la Iran
Moyo wa mapambano na kusimama kidete ni kielelezo cha heshima ya jeshi la Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumapili) ameonana na majimui ya makamanda na maafisa waandamizi wa kikosi cha majini cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuutaja moyo wa muqawama na kusimama kidete kuwa ndilo chimbuko la heshima na itibari viliyo nayo vikosi vya ulinzi vya Iran na kuongeza kuwa, kikosi cha majini cha jeshi kinapaswa kuimarisha nguvu zake za kijeshi wakati wote kulingana na zama.
Taifa la Iran halina haja ya kuaminiwa na Marekani
Taifa la Iran halina haja ya kuaminiwa na Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na wajumbe wa Baraza Kuu la Basiji na wawakilishi wa matabaka mbalimbali ya Basiji na huku akiashiria udharura wa kuwa na hisia za wajibu wa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu na ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu na kuwa na busuri na muono wa mbali kwamba ni nguzo mbili kuu za tafakuri wa kimantiki ya Basiji, ameishukuru timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na jitihada zake kubwa na kulipa kwake uzito wa hali ya juu suala hilo na kutotetereka katika mazungumzo hayo.
Matakfiri wanapigana na Waislamu badala ya kupambana na Wazayuni
Matakfiri wanapigana na Waislamu badala ya kupambana na Wazayuni
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo (Jumanne) amehutubia hadhara ya maulamaa, wanavyuoni, wasomi na wageni walioshiriki kwenye Kongamano la Kimataifa la Mirengo ya Kitakfiri kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu na kusema kuwa kufufuliwa makundi ya kitakfiri katika miaka ya hivi karibuni ni tatizo lililopandikizwa na mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa, kuanzisha mwamko wa kielimu, kimantiki na wa pande zote kwa ajili ya kung'oa mizizi ya mrengo unaowakufurisha Waislamu wengine, kuwazindua Waislamu kuhusu njama za siasa za kibeberu za kutaka kuhuisha mrengo huo na kulipa umuhimu mkubwa suala la Palestina ni miongoni mwa nyadhifa na wajibu mkubwa zaidi unaopeswa kupewa kipaumbele na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu.

Anwani zilizochaguliwa