Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Ayatullah Mishkini alikuwa shakhsia aliyekusanya mambo mengi
Ayatullah Mishkini alikuwa shakhsia aliyekusanya mambo mengi
Leo asubuhi (Alkhamisi), Hujjatul Islam Walmuslimin Mohammad Golpayegani, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesoma matini ya hotuba ya Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na...
Taifa lililo hai la Iran kamwe haliwezi kupigishwa magoti
Taifa lililo hai la Iran kamwe haliwezi kupigishwa magoti
Sambamba na kuwadia mwezi 13 Rajab na maadhimisho matukufu ya siku ya kuzaliwa Bwana wa wanaompwekesha Mwenyezi Mungu, Imam Ali (AS), maelfu ya watu wa matabaka tofauti hasa wananchi wa mkoa wa Ilam wa magharibi mwa Iran leo (Jumanne) wameonana na Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei...
Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran haipaswi kulegeza kamba hata kidogo
Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran haipaswi kulegeza kamba hata kidogo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano) ambayo imesadifiana na Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia nchini Iran ameonana na maafisa wa ngazi za juu pamoja na wataalamu bingwa na wasomi wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran na kusema kuwa, moja kati ya mafanikio muhimu zaidi ya maendeleo ya nyuklia ya Iran ni kutia nguvu moyo wa kujiamini kitaifa nchini na kuandaa mazingira ya kupatikana maendeleo ya kielimu katika sekta nyinginezo.
Fikra potofu za Magharibi kuhusu mwanamke zinapaswa kutupiliwa mbali
Fikra potofu za Magharibi kuhusu mwanamke zinapaswa kutupiliwa mbali
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na mamia ya akina mama bora na wasomi walioteuliwa kutoka kona mbalimbali za Iran na kulitaja suala la kuanzisha kituo kikuu kitakachofanya kazi hadi nje ya mihimili mikuu ya dola kwa ajili ya kupanga mikakati sahihi kuhusiana na kadhia muhimu ya mwanamke na familia, kuwa ni jambo la dharura.
Taifa la Iran limeonesha kuwa linaweza kumshinda adui chini ya kivuli cha umoja, imani na kusimama kidete
Taifa la Iran limeonesha kuwa linaweza kumshinda adui chini ya kivuli cha umoja, imani na kusimama kidete
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumatano alikutana na maelfu ya watu waliokwenda kutembelea maeneo ya operesheni za kuvunja mzingiro wa Abadan huko mashariki mwa Kawavan kusini mwa Iran na kusisitiza juu ya udharura wa kulindwa kumbukumbu, jihadi na kujitolea kwa wapiganaji wa Kiislamu katika maeneo mbalimbali wakati wa vita vya kujitetea kutakatifu.
Iran inapaswa kuwa na nguvu kubwa ya kutetea haki zake mbele ya madhalimu
Iran inapaswa kuwa na nguvu kubwa ya kutetea haki zake mbele ya madhalimu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Ijumaa) ambayo imesadifiana na siku ya kwanza ya msimu wa machipuo na siku ya awali kabisa ya mwaka mpya wa Kiirani wa 1393 Hijria Shamsia ametoa hotuba muhimu mbele ya hadhara na mjumuiko mkubwa na uliojaa hamasa na shauku wa wafanya ziara na majirani wa Haram toharifu ya Imam Ridha AS mjini Mash'had, kaskazini mashariki mwa Iran. Sambamba na kutoa tena mkono wa baraka kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya amebainisha pia vipengee mbalimbali vya ramani kuu ya njia kwa ajili ya Iran katika mwaka huu mpya yaani kaulimbiu ya "Uchumi na Utamaduni wenye Azma ya Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."
Hali ya watu maskini inapaswa kuboreshwa katika maendeleo ya kiuchumi
Hali ya watu maskini inapaswa kuboreshwa katika maendeleo ya kiuchumi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi (Jumanne) amebainisha muundo wa siasa za uchumi wa kimuqawama na imara mbele ya mjumuiko ya mamia ya wakuu na maafisa wa vyombo mbalimbali, wanaharakati wa masuala ya kiuchumi, wakuu wa vituo vya kielimu, vyombo vya habari na taasisi za usimamizi. Amesema kuwa kuna sababu, nia na msukumo na vilevile matarajio ya wananchi kutoka kwa viongozi na maafisa husika.
Viongozi wa Mfumo wa Kiislamu waweke wazi mpaka baina yao na kambi ya adui
Viongozi wa Mfumo wa Kiislamu waweke wazi mpaka baina yao na kambi ya adui
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na wajumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu) na kutoa hotuba muhimu. Amegusia baadhi ya matukio ya kimataifa na kuzungumza majukumu waliyo nayo viongozi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika wakati huu nyeti na tata.
Jamii yenye utamaduni ya kufa shahidi haiwezi kubakia nyuma
Jamii yenye utamaduni ya kufa shahidi haiwezi kubakia nyuma
Miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na wajumbe wa kamati za Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi, Kongamano la Mashahidi wa Wanachuo na Kongamano la Mashahidi Wasanii, imesambazwa leo asubuhi katika Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mnara wa Milad, jijini Tehran. Mkutano wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wajumbe wa kamati hizo ulifanyika tarehe 16 Februari 2015.
Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mabavu ya Marekani
Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mabavu ya Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia maelfu ya wananchi wa miji mbalimbali ya mkoa wa Azarbaijan Mashariki waliokwenda kuonana naye akilishukuru taifa la Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman (Februari 11) ya kuadhimisha miaka 35 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. Amesema maandamano hayo yalikuwa na ujumbe mbili ambazo ni kusimama kidete na umoja. Ayatullah Khamenei amesema taifa la Iran lilihudhuria kwa wingi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman katika kujibu ufidhuli, sera za kupenda kujitanua, utovu wa adabu na kiburi cha viongozi wa Marekani, na kutangaza kuwa kamwe halitasalimu amri mbele ya sera za mabavu za Marekani.
Uwezo mkubwa wa nchi hizi mbili unatayarisha uwanja wa kuimarisha uhusiano
Uwezo mkubwa wa nchi hizi mbili unatayarisha uwanja wa kuimarisha uhusiano
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Khamenei amesema udugu, upendo na urafiki uliopo hivi sasa kati ya Iran na Uturuki hauna kifani katika karne za hivi karibuni. Amesema kuwa uwezo mkubwa wa nchi mbili hizi unatayarisha uwanja mzuri wa kupanuliwa na kuimarisha uhusiano.
Umoja ndiyo suala muhimu zaidi la Ulimwengu wa Kiislamu
Umoja ndiyo suala muhimu zaidi la Ulimwengu wa Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapunduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo katika siku ya Maulidi na sherehe za kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) na mjukuu wake Imam Ja'far Swadiq (sa) alikutana na viongozi wa Mfumo wa Kiislamu wa Iran, wageni wanaoshiriki mkutano wa 27 wa Umoja wa Kiislamu na matabaka mbalimbali ya wananchi. Ameuhimiza Umma wa Kiislamu kutimiza matarajio ya Mtume Muhammad (saw) na kusema: Umoja ndiyo suala muhimu zaidi hii leo katika ulimwengu wa Kiislamu.

Anwani zilizochaguliwa