Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Tunapaswa kujitegemea katika nyanja zote za viwanda
Tunapaswa kujitegemea katika nyanja zote za viwanda
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amekagua moja ya viwanda vikubwa hapa nchini na kushuhudia kwa karibu sehemu ya uwezo wa kiviwanda wa taifa hususan katika sekta ya utengenezaji magari na uzalishaji wa injini ya kitaifa.
Katika ukaguzi huo ulioendelea kwa muda wa masaa matatu na kuhudhuriwa na mawaziri kadhaa na wakurugenzi wa sekta mbalimbali za viwanda na madini, wataalamu wa kiwanda hicho walitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu mwenendo wa uzalishaji kiwandani hapo.

Anwani zilizochaguliwa